DAR ES SALAAM: Mapema leo asubuhi, lori la maji taka limechafua hali ya hewa kwenye Barabara ya Morogoro baada ya kumwaga ‘mzigo’ (maji yenye kinyesi) katikati ya barabara hiyo maeneo ya Ubungo Mataa na kusababisha taharuki na harufu kali.
Kwa mujibu wa mshuhuda wa tukio hilo, inasemekana kuwa lori hilo lilikuwa likitokea maeneo ya Rombo Kimara ambapo baada ya kufika Ubungo kwenye mataa ya foleni, mfuniko wa tanki uliftyatuka ndipo likaanza kumwaga uchafu huo barabarani.
Baada ya kuona hali hiyo, dereva wa lori hilo alitoka mbio na kwenda kuziba eneo ambapo uchafu huo ulikuwa ukitoka.
Hata hivyo watumiaji wa barabara hiyo na wafanyabiashara wa eneo hilo hasa wamachinga wameshangazwa tukio hilo huku wakieleza kuwa ilitakiwa dereva na kondakta wa gari hilo wahakikishe mfuniko wa tanki umekaza kabla ya kuanza safari ili kuzuia ajali kama hizo ambazo zinaweza kuepukika kwa kuzingatia umakini wa kazi.
Aidha wananchi hao wameitaka Manispaa ya Jiji la Dar es Salaam imchukulie hatua zinazostahili mmiliki wa gari hilo na dereva wake ikiwa ni pamoja na kumtoza faini au kusafisha barabara kutokana na adha aliyoisababisha ili liwe funzo kwa wamiliki na madereva wengine wa magari ya maji taka.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment