» » Duh!! Umesikia Alichosema Niyonzima Juu ya Kocha Wake Lwandamina,Soma Hapa Kujua kama Yuko Sahii Kusema Haya Au Amerocharocha

 
Nahodha wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa anaamini kocha wao George Lwandamina atakipeleka mbali zaidi kikosi hicho kwenye michuano ya kimataifa na kutwaa ubingwa wa ligi kutokana na ubora wake na kudai kuwa kinachotakiwa apewe muda na si watu kuanza kumlalamikia kwa matokeo yoyote yatakayopatikana.

Kumekuwa na tuhuma kuwa Lwandamina amekuwa akiwapa mazoezi magumu wachezaji wake hadi siku ya mechi, hivyo kusababisha wachezaji hao kuchoka na kushindwa kufanya vyema kwenye mechi.

Niyonzima amesema kuwa, siyo wakati muafaka kwa sasa kutoa lawama kwa kocha huyo kwa kuwa bado hajakaa na timu kwa muda mrefu, hivyo anahitaji kuyasoma mazingira kisha ndipo aweze kufanya vyema.
 
“Lwandamina ni mwalimu mzuri na tunamuelewa sana tofauti na watu wanavyodhania, pia watu wanahitaji kutambua kuwa, kocha huyo anatakiwa apewe muda wa kutosha kuweza kuinoa timu hiyo na hasa ukizingatia yeye ni mgeni, hivyo hawezi kukopi kila kitu kwa wakati mmoja.

“Anatakiwa kupewa muda wa kuweza kuelewa kila kitu ndipo aweze kufanya kazi yake ipasavyo na si tuhuma ambazo amekuwa akipewa kwani naamini atatufikisha mbali zaidi kwenye ligi na mashindano ya kimataifa,” alisema Niyonzima.


Aidha, alimalizia kwa kusema kuwa, anaamini wataweza kufanikiwa kutetea ubingwa wa ligi kwa kuwa wamejiandaa vyema, licha ya kutambua kuwa mzunguko wa pili ni mgumu na wanahitaji kujipanga na kujituma ili waweze kufanikiwa kutetea taji lao hilo.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...