» » HAWA NDIO MABILIONEA NANE 8 WANAOMILIKI MALI ZA WATU BILION 3.7

Utafiti uliofanywa na shirika la Oxfam la Uingereza unaonesha mabilionea wanane wanamiliki mali sawa na mali ya watu 3.6 bilioni kwa pamoja.
Takwimu za shirika hilo, ambazo zimepingwa na baadhi ya wakosoaji, zinatokana na maelezo na habari za kina zilizokusanywa na shirika hilo, na zinaonesha pengo kati ya matajiri na maskini ni kubwa kuliko ilivyodhaniwa awali.
Ripoti hiyo ya Oxfam imetolewa wakati mkutano mkubwa kuhusu uchumi wa dunia unaanza mjini Davos. Mark Littlewood, wa Taasisi ya Masuala ya Uchumi, amesema Oxfam badala yake wanafaa kuangazia njia ya kusisimua ukuaji.
“Kama shirika linalopiga vita umaskini, Oxfam wanaonekana sana kuangazia zaidi matajiri,” Mkurugenzi mkuu huyo wa shirika hilo la ushauri amesema.
Kwa wale ambao wana malengo ya “kutokomeza kabisa umaskini uliokithiri”, sana wanafaa kuangazia hatua za kusisimua ukuaji wa uchumi, ameongeza.
Ben Southwood, ambaye ni mkuu wa utafiri katika Taasisi ya Adam Smith, amesema la muhimu zaidi si kiasi cha mali inayomilikiwa na watu matajiri zaidi duniani, bali ni hali ya maisha ya watu maskini zaidi duniani, ambayo inaimarika mwaka baada ya mwaka.
“Kila mwaka, tunapotoshwa na takwimu za Oxfam. Takwimu ziko sawa – zinatoka kwa Credit Suisse – lakini ufasiri wa takwimu hizo si sahihi.”
‘Mkutano wa Davos‘
Mkutano unaofanyika mjini Davis, Uswizi huwavutia viongozi wengi wa kisias ana kibiashara duniani.
Katy Wright, mkuu wa mambo ya nje wa Oxfam, anasema ripoti hiyo imesaidia shirika hilo kuwauliza maswali viongozi wa kisiasa na kiuchumi.
“Tuna uhakika kwamba Davos ni mkutano tu mwingine wa kupiga gumzo miongoni mwa viongozi na watu wenye ushawishi duniani, lakini tunahitaji kujaribu na kupata mwelekeo,” aliongeza.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...