Zitto ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini ametoa msimamo wa kujiuzu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook na Twitter.“Serikali ya CCM ikinionesha tani 1.5 milioni za chakula ambazo inataka kusambaza, najiuzulu Ubunge mara moja. Narudia, mpaka Oktoba 2016 kulikuwa na nafaka tani 90,400 tu kwenye maghala yote ya NFRA.
“Tunashukuru kuwa Hivi sasa ajenda ya tishio la njaa inapata majawabu na matamko. Ndio wajibu wa vyama vya siasa. Kuibua masuala muhimu kwa nchi yetu,” ameandika Zitto.
Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo ya nchi, zimeripotiwa taarifa za kuwepo kwa uhaba wa chakula unaotokana na ukame kiasi cha kusababisha vifo vya mifugo kwa kukosa malisho.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment