» »Unlabelled » Kiir akubali wanajeshi wa UN watumwe Juba, Sudan Kusini

Kiir akubali wanajeshi wa UN watumwe Juba, Sudan Kusini


Mshirikishe mwenzako
Wanajeshi wa UNImage copyrightAFP
Image captionWanajeshi hao wapya watatoka Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan na Uganda
Rais wa Sudan Kusini hatimaye amekubali kikosi cha ziada cha wanajeshi wa kulinda amani kitumwe nchini humo.
Rais Salva Kiir alichukua hatua hiyo baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Bw Kiir alikuwa awali amekataa kutumwa kwa wanajeshi hao 4,000 kutoka mataifa ya kanda, akisema huo ni ukiukaji wa uhuru wa Sudan Kusini.
UN iliidhinisha kutumwa kwa wanajeshi hao baada ya kuzuka upya kwa vita baina ya wanajeshi waaminifu kwa Bw Kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Dkt Riek Machar mwezi Julai mjini Juba.
Kikosi hicho cha ziada kitakuwa na mamlaka zaidi kushinda kikosi cha sasa cha wanajeshi 13,000 ambacho kimekuwa kikihudumu nchini humo.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles