» »Unlabelled » Hatimaye Rousseff aenguliwa rasmi madarakani

Hatimaye Rousseff aenguliwa rasmi madarakani


Mshirikishe mwenzako
Dilma RousseffImage copyrightAFP
Image captionDilma Rousseff
Rais Mpya wa Brazil Michel Temer amesema nchi yake inaingia katika enzi mpya ya matumaini baada ya kuondoshwa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff.
Akizungumza na taifa hilo kupitia Televisheni, Rais Temer ametoa wito wa kuungana pamoja na kusema kuwa kuondolewa madarakani kwa bibi Rousseff kumemaliza miezi kadhaa ya mashaka.
Wabunge nchini humo walipiga kura ya kutokuwa na imani na Bibi Rousseff ya kumuondoa madarakani kwa asilimia 61 huku kura 20, zikipinga kuondolewa kwake.
Amekutwa na hatia ya udanganyifu wa bajeti ya nchi hiyo wakati wa kampeni zake za uchaguzi muiaska miwili iliyopita.
Makamu wa rais , Michel Temer ambaye amemrithi Bi Rousseff kwa muda, amekula kiapo cha urais hadi ifikapo January 2019.
Katika majibu yake ya kwanza ya kura zilizopigwa, Bi Rousseff amesema kuwa, Baraza la Seneti halikutenda haki kwa mwanamke asiye na hatia.
Aidha amewashutumu Maseneta ambao walipiga kura ya kumuondoa madarakani kwamba wamehusika katika mapinduzi ya kisiasa.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...