» »Unlabelled » Fujo Gabon baada ya Bongo kutangazwa mshindi

Fujo Gabon baada ya Bongo kutangazwa mshindi


Mshirikishe mwenzako
Majengo ya bunge mjini LibrevilleImage copyrightAFP
Image captionMajengo ya bunge mjini Libreville yamechomwa moto na waandamanaji
Fujo zimezuka katika mji mkuu wa Gabon, Libreville baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi.
Mgombea wa upinzani Jean Ping amesema watu wawili wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya vikosi vya usalama kuvamia makao makuu ya chama chake.
Serikali imesema inawaandama "wahalifu wenye silaha" ambao awali walikuwa wameteketeza majengo ya bunge.
Bw Ping amepinga matokeo ya urais ambayo yalionyesha Rais Bongo alishinda uchaguzi kwa kura chache. Hii inampa fursa ya kuongoza taifa hilo kwa muhula mwingine wa miaka saba.
"Walishambulia mwendo wa saa 01:00 (00:00 GMT). Ni kikosi cha wanajeshi walinzi wa rais. Walikuwa wanarusha mabomu kutoka kwa helikopta na kisha baadaye wakashambulia kutoka ardhini," Bw Ping, ambaye hakuwa katika makao makuu hayo wakati huo, alisema awali.
Ameomba usaidizi kutoka kwa jamii ya kimataifa kulinda raia.
Wafuasi wa Bw Ping walikabiliana na polisiImage copyrightAFP/GETTY
Image captionWafuasi wa Bw Ping walikabiliana na polisi
Wafuasi wa Jean PingImage copyrightAFP/GETTY
Wanajeshi waliitwa kukabiliana na waandamanajiImage copyrightAFP/GETTY
Image captionWanajeshi waliitwa kukabiliana na waandamanaji
Matokeo ya uchaguzi yalitangazwa Jumatano alasiri na kumpatia Bw Bongo ushindi kwa 49.8% ya kura, akifuatwa na Bw Ping aliyepata 48.2 % ya kura, kura zilizowatenganisha zikiwa 5,594.
Bw Ping alisema uchaguzi huo ulijaa udanganyifu na "hakuna ajuaye" hasa nani alishinda.
Waandamanaji waliingia barabarani muda mfupi baada ya tangazo kutolewa. Walichoma moto majengo ya bunge na kukabiliana na polisi wa kuzima fujo.
Upande wa Bw Ping unasema takwimu kutoka ngome za rais huyo zinaonyesha asilimia 99 ya wapiga kura walijitokeza. Ameomba takwimu za wapiga kura kutoka kila kituo zitolewe wazi.
Ramani ya Gabon
Marekani na Umoja wa Ulaya wametoa wito kura hizo ziwekwe wazi huku katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon naye akihimiza utulivu.
Bw Bongo aliingia madarakani mwaka 2009, baada ya kifo cha babake aliyechukua madaraka 1967.
Kabla ya kuingia kwenye siasa, Bw Ping alikuwa mwanadiplomasia ambaye alihudumu kama mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Bw Ping alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa AfrikaImage copyrightAFP
Image captionBw Ping alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika
Ali BongoImage copyrightAFP/GETTY
Image captionBw Bongo aliingia madarakani mwaka 2009

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...