Zaidi ya Watu 40,000 wanashikiliwa Uturuki
Waziri Mkuu wa
Uturuki, amesema zaidi ya watu 40,000 wanashikiliwa na Polisi
wakihusishwa na jaribio la kuipindua Serikali ya nchi hiyo.
Katika
hotuba yake ya moja kwa moja katika Televisheni, Binali Yildirim pia
alisema takriban wafanyakazi wa sekta ya Umma 80,000 wamefutwa kazi
wakiwemo wanajeshi,Polisi na watumishi wa Umma.Maelfu ya Taasisi yameshukiwa kuwa na mahusiano na Kiongozi wa kidini, Fethullah Gulen zimefungwa.
Serikali ya Uturuki imemshutumu Gulen, ambaye anaishi uhamishoni nchini Marekani kwa kusuka mipango ya mapinduzi .
Awali, Serikali ya Uturuki ilisema itawaachia huru watu 30,000 ili kupunguza mrundikano kwenye magereza.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment