Miongoni mwa habari kuu leo,
wazima moto 10,000 wanakabiliana na moto uliozuka karibu na mji wa San
Bernardino, California na ubaguzi dhidi ya watu weusi Uingereza
umeongezeka.
1. Wazimamoto 10,000 wakabiliana na moto California
Image caption
Moto huo umeathiri maelfu ya watu kusini mwa jimbo la California
Zaidi ya watu 10,000 wanashiriki katika juhudi za
kukabiliana na moto katika jimbo la California ambako kumezuka msururu
wa visa vya moto katika maeneo manane.
Maafisa wa kikosi hicho maalumu cha kukabiliana na moto wanasema kuwa sehemu moja kulikozuka moto kumewashinda wahusika kuuzima.
Moto huo umelazimisha kufungwa kwa barabara na reli inayounganisha miji ya Los Angeles na Las Vegas.
2. Ubaguzi dhidi ya weusi Uingereza waongezeka Ripoti mpya nchini Uingereza imeonya kuwa watu weusi
na wale wanaotoka jamii za watu wachache wanakabiliana na kile
kilichotajwa kama ubaguzi uliokubalika katika maeneo mengi.
Inadaiwa
kuwa hali hiyo imekuwa mbaya zaidi kwa muda wa miaka mitano iliyopita.
Ripoti hiyo iliyotolewa na Tume ya Usawa na Haki za Kibinadamu inaeleza
masikitiko yake juu ya ongezeko maradufu la makosa ya chuki tangu
Uingereza kupiga kura kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya mnamo Juni.
Serikali imesema itaupiga msasa mpango wa haki hivi karibuni.
3. Rais wa Bolivia kufungua chuo cha kushindana na Marekani Rais wa Bolivia, Evo Morales, amefungua rasmi chuo
maalumu cha kijeshi kinachotoa mafunzo yanayoshindana na yale
yanayotumiwa na Marekani kujiimarisha katika mataifa yanayostawi
duniani. Bw Morales alisema kuwa chuo hicho kipya kinakusudia kushindana
na kile kijulikanacho kama US Army of the Americas kilichokuwa kikitoa
mafunzo kwa washirika wa Marekani katika Vita Baridi katika eneo la
Latin America.
4. Watu watatu wauawa kwenye shambulio Uturuki ANADOLU AGENCYSerikali ya Uturuki inasema watu watatu wameuawa na
wengine 40 kujeruhiwa katika bomu lililotegwa katika gari la kulipuliwa
karibu na kituo cha polisi na kambi ya jeshi Mashariki mwa Van, karibu
na mpaka na Iran.
Picha katika runinga zinaonyesha magari kadhaa
ya polisi na ambulansi katika eneo hilo. Haikujulikana mara moja
aliyehusika katika shambulio hilo. 5. Cisco kuwafuta kazi wafanyakazi
Kampuni kubwa ya utengenezaji wa vifaa vya kiufundi,
Cisco systems, imetangaza mipango ya kuwafuta kazi asilimia saba ya
wafanyakazi wake kote duniani, huku ikibadilisha aina ya vifaa
inavyotengeneza; kulenga biashara inayozidi kuimarika zaidi katika sekta
za usalama na teknolojia ya kikompiuta.
Kupitia taarifa maalumu Cisco wamesema kuwa watawaachisha kazi watu 5,500.
Mshirikishe mwenzako
Pakua App Yetu-Bofya Hapa
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share !
Topics:
About 4sn News
Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
No comments:
Post a Comment