» »Unlabelled » Trump kuzuru Mexico licha ya msimamo mkali

Trump kuzuru Mexico licha ya msimamo mkali


TrumpImage copyrightAP
Image captionKwenye kampeni, Bw Trump amewaeleza wahamiaji wa Mexico wanaoingia Marekani kama "wahalifu" na "wabakaji"
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amekubali mwaliko wa kumtembelea rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, Jumatano.
Afisi ya rais huyo imesema mipango ya kufanyika kwa mazungumzo ya faraghani baina ya wawili hao inakaribia kukamilishwa.
Mkutano huo utafanyika muda mfupi kabla ya Bw Trump kutoa hotuba kuhusu uhamiaji nchini Marekani.
Kwenye kampeni, Bw Trump amewaeleza wahamiaji wa Mexico wanaoingia Marekani kama "wahalifu" na "wabakaji".
Ameahidi kujenga ukuta kuwazuia wahamiaji hao kuingia nchini humo iwapo atachaguliwa kuwa rais.
MexicoImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionTrump pia ametishia kuzuia raia wa Mexico walio Marekani wasitume pesa nyumbani
Rais Pena Nieto pia ametoa mwaliko kwa mgombea urais wa chama cha Democratic Bi Hillary Clinton.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles