Wajasiriamali wadogowadogo na wa kati
kuchangia kiasi kikubwa kwenye kuongeza ajira,kuongeza kipato na
kuchochea ukuwaji katika maeneo ya mijini na vijijini.inakadiriwa kwamba
kiasi cha theluthi moja ya pato la taifa[GDP] inatokana na sme kwa
mujibu wa utafiti wa sekta isiyo rasmi wa mwaka 1991 wajasiriamali
wadogo wadogo wanaoendesha shughuli katika sekta isiyo rasmi. Pekee na
zaidi ya biashara milioni 1.7 zinazo waajiri watu milioni 3 ambayo ni
sawa na asilimia 20% ya wafanyakazi mahiri Tanzania
Wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati
[SME's] wanatoa mchango mkubwa sana katika kutoa ajira na kuongeza
kipato nchini Tanzania SME duniani kote na hasa Tanzania, zinaweza
kuanzishwa kwa urahisi kwa sababu masharti yake kwa upande wa mtaji,
tekinolojia, usimamizi na hata miundombinu [maji, umeme, simu] si muhimu
sana kama ilivyo katika shughuli kubwa .Shughuli hizi za wajasiliamali
wadogo na wakati zinaweza kuanzishwa hata vijijini na hivyo kuongeza
thamani kwa bidhaa za kilimo nawakati huwohuwo uwezesha kuenea kwa
shughuli hizo. Kwa hakika uendelezaji wa SME unahusiana kwa karibu
zaidi na usambazaji wa mapato kwa usawa na haki zaidi na hivyo muhimu
kwa kupunguza umasikini wakati huwohuwo SME nikama eneo la kujifunzia
kwa wajasiriyamali wanao chipukia.
Sekta ya SME inaongozwa na Sera ya Maendeleo ya Wajasiriyali Wadogowadogo na wa Kati ya mwaka 2003
kushughulikia vikwazo na kutumia kwa ukamilifu uwezo wa sekta, inakuwa
kama muongozo elekezi kwa wadau wote na hivyo kuchochea kuanzishwa kwa
shughuli mpya na zilizopo kukua na kuwa zaushindani zaidi.
MPAKA HAPO UNASUBIRI NINI KUWA MJASIRIAMALI?
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment