» » SOMO; "KWA NINI TUNAKUFA?"


Jibu liko wazi kabisa kwamba kufa kwetu Ni matokeo ya dhambi...
 Kile walichofanya wazazi wetu wa kwanza kwa kushindwa kutii Sheria ya Mungu yenye upendoπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Mwanzo 2:17
[17]walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Kifo kinachozungumziwa hapa Ni kifo Cha milele, Mwanadamu alipotenda dhambi na ilibidi afe ili kuilipia dhambi, kumbuka kuwa mshahara wa dhambi Ni mauti.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ Anagalia hii
Warumi 5:12,14
[12]Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
[14]walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.

Lakini pamoja na hayo habari njema NI hii Yesu alikuja ili kulipa Deni la dhambi hii akafa kifo ambacho adamu na uzao wake wote ilibidi wapitie Yaani kifo Cha milele. πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ Angalia hii
Warumi 5:17-18
[17]Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.
[18]Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.

Kwa maana hiyo, kila amwaminiye Yeye Basi atakuwa amelala usingizi tu na Yesu atakapokuja ataamshwa ...Hivyo kwa tunaomwamini Yesu Leo tukifa ni usingizi tu Angalia hii πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

1 Wakorintho 15:20-23
[20]Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.
[21]Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.
[22]Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.
[23]Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.


Mungu awabariki Sana. Ni Mimi Pr Sanida Musa mtumishi niliye mdogo kabisa.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...