*SOMO: KATIKA UGONJWA NA KATIKA AFYA (ISAYA* 38, 39)
Matukio ya Isaya 38 na 39 (2 Wafalme 20) yalitokea kwa karibu sana na wakati Mungu alipomwokoa Hezekia kutoka kwa Senakeribu, ijapokuwa wokovu, kama ilivyoelezwa katika Isaya 37 (tazama pia 2 Wafalme 19) ulikuwa haujatokea. Kwa hakika, Isaya 38:5, 6 na 2 Wafalme 20:6 huonesha kwamba bado walikabiliwa na kitisho cha Ashuru.
"Shetani alikuwa amekusudia kusababisha kifo cha Hezekia pamoja na kuiangusha Yerusalemu, akiamini kwamba ikiwa Hezekia atatoweka, jitihada za matengenezo zingekoma na anguko la Yerusalemu lingekamilishwa haraka" —The SDA Bible Commentary, vol. 4, uk. 240.
Nukuu hapo juu hutuambia nini kuhusu umuhimu wa uongozi mzuri kwa watu wa Mungu? Ni ishara gani Bwana anampatia Hezekia kuithibitisha imani yake? 2 Wafalme 20:8-10; Isa. 38:6—8
Kwa kuzikataa ishara zilizotolewa na Mungu (Isaya 7), Ahazi alikuwa ameanzisha mwelekeo wa matukio ambayo yaliwaweka katika matatizo na Ashuru. Lakini sasa Hezekia aliomba ishara (2 Wafalme 20:8); hivyo, Mungu anamtia nguvu kulikabili tatizo ambalo Baba yake aliiletea Yuda. Kwa hakika, kurudisha nyuma kivuli katika saa ya Ahazi ilikuwa inawezekana tu kwa muujiza.
Wababeli walijifunza nyendo za sayari, jua, mwezi na nyota na kuziwekea kumbukumbu kwa usahihi. Hivyo, waliweza kutambua mwendo wa jua usiokuwa wa kawaida na kushangaa ulimaanisha nini. Ukweli kwamba mfalme Merodak-baladani aliwatuma wajumbe kwa wakati huu si wa bahati mbaya. Wababeli waligundua muunganiko kati ya kupona kwa Hezekia na ishara hii ya ajabu.
Sasa tunajua kwa nini Mungu alichagua ishara hii. Kama vile baadaye alivyotumia nyota ya Bethlehemu kuwaleta mamajusi toka Mashariki. Hii ilikuwa fursa ya kipekee kwao kujifunza kuhusu Mungu wa kweli. Merodak-baladani aliutumia muda wote wa maisha yake akijaribu kujipatia uhuru wa kudumu kutoka kwa Ashuru. Alihitaji ushirika hodari, unaoelezea dhamira yake ya kuwasiliana na Hezekia. Ikiwa jua lenyewe lilisogea kwa ombi la Hezekia, angewafanyia nini Ashuru?
Ni kwa namna gani Hezekia alipoteza fursa ya kipekee ya kumtukuza Mungu na kuwaelekeza Wababeli kwake? Matokeo yalikuwaje? Isaya 39. Hezekia ambaye alipaswa kuwashuhudia kuhusu Bwana, alielekeza, badala yake kwa utukufu wake mwenyewe.” Tunajifunza nini hapa?
*KATIBUNI NYOTE KWA MJADALA WA LESSONI*
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment