NENO WOKOVU(SALVATION) Ni Kama gari ambalo ndani yake Lina abiria na bado halijafika katika kituo Cha mwisho, watu wengi watashuka njiani na wengine kuendelea na Safari, kushuka kwa baadha ya abiria njiani haimaanisha kuwa gari limefika mwisho, Bali linaendelea na Safari.
πππ Je naamisha Nini?
Neno WOKOVU Lina vitu vingi ndani yake. Baadha yake yameshatimilika, kutimilika kwake Haina maana kwamba wokovu umekamilika japokuwa mchakato unaendelea.
1. Ndani ya wokovu Kuna ukombozi (Redemption) hii aliikamilisha Yesu msalabani Mwanadamu akakombolewa katika kutoka mikononi wa Adui shetani. Yesu aliotamka tu kwamba imekwisha ukombozi ukawa umekamilika, shetani Leo Hana uwezo Tena wa kutushinda Ila tunamshinda pale tu tunapolitaja jina la Yesu.
2. Ndani ya wokovu kuna kuongoka. Kuongoka Ni pale tu mtu anapogeuka na kuacha nuia zake mbaya, kuongoka humaanisha "kugeuka" na hii Ni kukubali kumpa Yesu maisha yako yote na kuacha nuia zako ambazo hazimpendezi Mungu.
3.Ndani ya wokovu Kuna kuhesabiwa haki kwa Imani(Justification) tunahesabiwa haki kwa Imani si kwa matendo yetu mazuri, Bali Ni kwa Neema ya Yesu aliyetukomboa.
Je Kama Ni kwa Neema je tuendelee kutenda dhambi??
πππWarumi 6:1-3
[1]Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
[2]Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
[3]Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
4. Ndani ya wokovu Kuna utakaso (Sanctification) utakaso Ni kile kile kitendo Cha kumrudia Mungu kwa njia ya Toba kila siku, hii humaanisha kwamba sisi hatujakamilika. Angalia hiiπππ
Warumi 3:23-24
[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
[24]wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
Hivyo dhambi hii husafishwa kupitia utakaso kwa jina la Yesu πππ
Nyongeza ya Hiloπππππ
1 Yohana 2:1-2
[1]Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
[2]naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
Huo huotwa utakaso wa kila siku,
Siku tukitambua kuwa hakuna aliyekamilka hapa duniani Ila yupo anayekamilishwa kila siku hatutadharau na kuwahukumu wadhambi, Bali tutawaelekeza kwa yeye anayeweza kukamilisha hao wadhambi ambaye Ni Kristo Yesu pekee. Hukumu tumwachie Mungu maana yeye ndiye ajuaye wokovu wa mtu.
Hivyo tusipende kuhitimisha wokovuπππ Nyongeza ni hii ,πππ
2 Petro 2:20
[20]Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
Tuwe makini Sana kuhitimisha kuwa kukamilika kwa wokovu wetu.... ...... Huku tukisahau Kuna kuanguka na kunaswa, lakini Neema ya Yesu yatosha maana kwa uwezo wetu hatuwezi.
Namaliziaππππππ
5.Jambo la mwisho katika wokovu Ni kuchukuliwa kwenda mbinguni (Glorification) hii ndiyo hatua ya mwisho kabisa ya wokovu wa Mwanadamu ambapo dhambi haitakuwepo Tenaπππ Ona hii.
1 Wakorintho 15:53-56
[53]Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
[54]Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
[55]Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?
[56]Uchungu wa mauti ni dhambi........... Hapo wokovu utakuwa umekamilika Kama Ni gari litakuwa limefika kwenye kituo Cha mwisho.
Mungu atusaidie tuelewe hili fundisho vizuri kwa jina la Yesu amen. πππ
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment