Asili ya hii sikukuu Ilianzishwa huko Rumi(Italia ya Sasa) mnamo karne ya tatu yaani mwaka wa 300 baada ya kristo.
MWANZILISHI wa hii sikukuu alikuwa Padri Valentinus aliyekuwa kiongozi wa dini ya Rumi(Roman Catholic ya sasa)na alianzisha hii siku akiwa gerezani ambapo alihukumiwa na kiongozi wa serikali ya kirumi kaisari aliyeitwa Claudius II, ambaye alipitisha Sheria ya Askari wa kirumi kutokuoa wala kuolewa akiamini watakuwa wakakamavu vitani. Sasa Padri Valentinus aliendelea kufungisha ndoa kwa Askari akidai huwezi kuwazuia wapendanao. Hicho kikawa chanzo Cha yeye kwenda gerezani. Inasadikika alihukumiwa tarehe 14 February.
Sasa baada ya kaisari Claudius II kupiga marufuku kuoa na kuolewa na Askari wa Rumi. Pakawa na ongezeko la zinaa na ngono zembe katika taifa la Rumi. Na watu walikuwa wakimkumbuka Sana Padri Valentinus kila ifikapo tarehe 14 February wakidai alitetea maslahi ya wapendanao na kwa kulitimiza hilo walifanya uzinzi kupita kawaida, wanafunzi walipewa mimba na ndoa nyingi zilikuwa zikiharibika kutokana na watu kuchepuka wakidai wanasherekea sikukuu ya wapendanao....Mambo haya yalifanyika kwa kificho wakiogopa amri ya kaisari.
Sasa katika ULIMWENGU wa roho tayari hiyo sherehe inaunganishwa na madhabahu ya uzinzi. Jini mahaba, jini maimuna, roho ya Yezebeli na mapepo ya uzinzi huwa yanafurahi Sana siku hii maana yanapata nafasi ya kualikwa na WANADAMU ili kuadhimisha siku hii. Jambo ambalo mpaka Sasa linaendelea.
Fuatilia Sana Mambo yanayofanyika siku ya valentine unakuta uzinzi unaenezwa Sana, wengi wamepata UKIMWI wa kipepo bila kujua na wengi wameitolea sadaka mapepo ya zinaa ndani ya siku hii pasipo kujua. na Mambo mengi machafu hufanyika siku ya sikukuu hii.
KIFUPI NI KWAMBA UNAPOSHEREKEA SUKUKUU HII UNAJIUNGANISHA NA ROHO ZA UZINZI NA UASHERATI BILA WEWE KUJUA MATOKEO YAKE NI NDOA KUVUNJIKA, KUCHELEWA KUOA AU KUOLEWANA WAKATI MWINGINE UNAWEZA UKAKOSA KUOLEWA KABISA MAANA UNAKUWA TAYARI UMEOA JINI AU UMEOLEWA NA JINI MAHABA KUPITIA SIKUKUU ZA KIPEPO KAMA HIZI
.
EV DANIEL
BARIKIWA NA BWANA YESU ALIYE HAI
USIJE SEMA HUKUAMBIWA.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment