» » KESHA LA ASUBUHIAlhamisi 11/02/2021


*WEMA WA MUNGU WAONESHWA* 

*Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.* 1Petro 2:9 

📜 Kama vile nta inavyoganda kifanani cha muhuri, ndivyo nafsi upokea na kuhifadhi sura ya uadilifu wa Mungu. Tunajazwa na kubadilishwa kwa kuutazama usafi na haki yake. Nafsi zetu zitakuwa goigoi na imani zetu zitanyong’onyezwa ikiwa hatutachochea na kuwa na imani imara, thabiti na hai... 

📜 Dhambi kubwa ya watu wa Mungu kwa wakati wa sasa ni, hatutambui thamani ya baraka ambazo Mungu ametupatia. Tunamtumikia Mungu na moyo uliogawanyika.Tunahifadhi kwa upendo mkubwa sanamu fulani na kuabudu katika hekalu lake. Kweli ya Mungu ni ya adili na takatifu, hutakasa nafsi, ikiwa italetwa katika maisha na kufumwa pamoja na tabia. 

📜 Mungu anatutafuta na kweli yake kututenga na kutufanya watu wa milki yake. Huu ni mvuto wa kweli. Uti wetu na kujitoa kwetu havilingani na nuru yetu na fursa zetu, na wajibu mtakatifu ulio juu yetu wa kutembea kama watoto wa nuru hatuutimizi. Kama Wakristo tunashindwa kufikia kiwango cha wito wetu mkuu. Maonyo na malaumu yametolewa kwetu na Mungu lakini yamekuwa na mvuto kwetu kwa muda tu kwa kuwa hatuizingatii kama kazi yetu ya maisha yote kusonga mbele kuelekea juu kuifikia mede ya thawabu ya wito mkuu katika Kristo Yesu. 

📜 Ikiwa watu wa Mungu wangezingatia manufaa yao bora, na kuelewa toka katika nuru ya Neno la Mungu kwamba tutahukumiwa kulingana na nuru iangazayo katika njia yetu. fadhila na fursa zote tulizopewa na Mungu ni kwa kusudi la kutufanya wanaume na wanawake bora. Watu wa Mungu sharti watoke katika kanuni walizozizoea, wakiifanya kuwa kanuni yao ya kwanza kuutafuta ufalme wa Mungu na haki yake na kisha kuzidi kukua toka nuru hadi nuru kubwa zaidi... 

🔘 *Kila mtu anayeamini Neno la Mungu kwa hakika ataonesha vile vile kwa kazi zake. Wema mkuu wa Mungu umeoneshwa katika mapenzi yake. Lolote ambalo mapenzi yake au Neno lake huwataka walifanye hawawezi kuwa Wakristo kama watapuuza kulifanya. Kweli inaweza kuokoa nafsi zetu, kwa kuwa Mungu kwa Roho yake mwenyewe ni wakala wa kudumu katika hilo, na uwakala wa kiungu huifanya kweli nguvu inayotakasa.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...