*AHADI YA UWEPO WAKE*
*Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.* 2Timotheo 4:2
📚 Yeyote anayejaribu kufanya kazi ya matengenezo ni lazima atakutana na upinzani mkali. Kazi hii inahitaji kujikana nafsi. Hatupaswi kuuliza ikiwa tunatambuliwa au hatutambuliwi. Kwa hili tunafanya kazi bure. Tazama namna ambayo Kristo alifanya kazi. Yeyote anayejaribu kazi yoyote ya matengenezo, yeyote anayejaribu kumwongoza mwenye dhambi katika maisha ya kujikana nafsi na utakatifu atahitaji kila saa uhakikisho uliotolewa na Kristo baada ya kufufuka kwake, “Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” (Mathayo 28:20).
📚 Lipokee Neno. Liishi Neno. Lihubiri Neno, kama ulivyofanya wakati uliopita. Bwana Yesu amekupatia ahadi ya uwepo wake. Ipokee; ithamini. Si kazi yako wala yangu kupima utambuzi unaooneshwa kwa ajili ya kujikana nafsi na kafara iliyotolewa.
📚 Kazi ya matengenezo itahitaji imani yote na machozi na maombi ambayo akili ya kibinadamu inaweza kustahimili. Agizo letu ni, inua msalaba, na uubebe ukimfuata Yesu, ukipambana sana kwa ajili ya roho ile ile iliyomfanya Yesu aonee shauku ubatizo wake alioutazamia wa kuteseka msalabani.
📚 Akiwa katika bustani ya Gethsemane, kikombe cha mateso kiliwekwa katika mikono ya Mwokozi, wazo lilimjia, Je, akinywee au auache ulimwengu kupotea dhambini? Mateso yake yalikuwa makubwa kiasi cha kushinda uelewa wa mwanadamu. Wakati ambapo maumivu ya moyo yalipomjia, “hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka chini” (Luka 22:44). Kikombe cha siri kilitikisika katika mkono wake. Katika zahama hii ya kuogofya, wakati kila kitu kikiwa hatarini, malaika mkuu asimamaye katika uwepo wa Mungu, alikuja pembeni mwa Kristo, si kukichukua kikombe toka mikononi mwake, bali kumhimiza akinywee, akiwa na uhakikisho wa upendo wa Baba.
🔘 *Kristo alikinywea kikombe, na hii ndiyo sababu wenye dhambi wanaweza kuja kwa Mungu na kupata msamaha na neema. Lakini wale wanaoshiriki katika utukufu wa Kristo ni lazima washiriki pia mateso yake... Je, tutabeba msalaba, na kwa akili tuelewe kile ambacho kumfuata Kristo humaanisha, tukiishi kwa kujikana nafsi katika kila hatua?*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment