📝Ni kwa namna gani usemaji mahiri wa amiri wa mfalme wa Ashuru ulimwathiri Hezekia na viongozi wake? 2 Wafalme18:37—19:4, Isa. 36:21—37:4.
📖Akiwa ametikiswa sana na kuomboleza katika taabu, Hezekia alimgeukia Mungu, akitafuta kwa unyenyekevu maombezi ya Isaya, nabii yuleyule ambaye baba yake aliyadharau mashauri yake.
🕹️Mungu alimtia shime Hezekia kwa namna gani? Isa. 37:5—7.
📖Ujumbe ulikuwa mfupi, lakini wa kutosha. Mungu alikuwa upande wa watu Wake. Isaya alitabiri kwamba Senakeribu angesikia tetesi ambayo ingemwondoa katika uvamizi wake wa Yuda. Hili lilitimizwa mara moja.
📖Akiwa amekatishwa tamaa kwa muda, lakini pasipo kuvunjika moyo, Senakeribu alimtumia Hezekia ujumbe wa vitisho: " 'Mwambieni Hezekia, mfalme wa Yuda, maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema, Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru.... Je, Miungu ya mataifa, ambao baba zangu waliwaangamiza, wamewaokoa (Isa. 37;10, 12, tazama pia 2 Nyakati 32:17) Mara hii Hezekia alienda moja kwa moja hekaluni na kuufungua ujumbe ule mbele za Bwana wa majeshi, " 'akaaye juu ya makerubi' " (Isa. 37:14—16).
📝Ni kwa jinsi gani ombi la Hezekia lilitambulisha kile kilichokuwa hatarini katika tatizo la Yerusalemu? Isaya 37:15—20.
📝Senakeribu alikuwa amelenga mashambulizi yake katika ngome imara kabisa ya Hezekia: imani kwa Mungu wake. Badala ya kuzungumza akiwa amejificha, Hezekiah alimlilia Mungu kudhihirisha ukuu wake “ ‘falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa Wewe ndiwe BWANA, wewe peke yako’ ” (Isa. 37:20).
🕹️Soma kwa maombi sala ya Hezekia (Isa. 37:15—20). Ni vipengele gani juu ya Mungu anavyovilenga? Je, tunaona kanuni gani katika ombi hili inayoweza kututia moyo na nguvu kudumu katika uaminifu tuwapo katika zahama?
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment