*MAISHA MAPYA*
*Akamwambia mfano mwingine, Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu ya unga, hata ukachachwa wote pia.* Mathayo 13:33
☄️ Chachu inapotiwa katika chakula, inapenya kila sehemu, hadi badiliko linapotokea kote. Ndivyo ilivyo kwa kazi ya Roho Mtakatifu katika moyo wa mwanadamu. Ukweli uliopokelewa na kuaminiwa huanzisha sheria mpya, kanuni mpya ya utendaji katika maisha. Kiwango kipya cha tabia huanzishwa —maisha ya Kristo. Wale ambao hupokea kweli humtegemea Kristo, nao hupokea nguvu nyingi zaidi, na nuru kubwa zaidi. Kila siku huondoa mioyoni mwao ubatili, ubinafsi na kujihesabia haki wenyewe.
☄️ Wanavyompokea Roho wa Kristo, nuru huangaza toka kwao miale angavu na dhahiri. Kuna kufanywa upya akili na moyo wote. Kama ambavyo chachu inayowekwa katika chakula huchachua chakula chote, ndivyo chachu ya kweli, ikitiwa moyoni, itasharabu sifa zote za roho, mwili, na moyo...
☄️ Badiliko la moyo humaanisha badiliko lote la mwanadamu kwa ujumla. “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu,” alisema Yesu (Yohana 3:3). Hili badiliko la moyo halionekani; kwa kuwa ni kazi inayotendeka ndani, na bado, linaonekana, kwa kuwa hufanya kazi kwa nje tokea ndani. Je, chachu ya kweli imetenda kazi katika moyo wako? Je, imesharabu moyo wote, mapenzi yote kwa nguvu yake inayotakasa?
☄️ Kazi yetu ya kwanza ipo katika mioyo yetu wenyewe. Kanuni za kweli za matengenezo ni lazima zifanyiwe kazi. Moyo ni lazima uongolewe na kutakaswa vinginevyo hatuna muunganiko na Kristo. Wakati mioyo yetu inapogawanyika, hatutafanywa kamwe tufae kwa kuwa wenye manufaa katika maisha haya na maisha yajayo. Kama viumbe wenye utambuzi, tunapaswa kukaa chini na kutafakari kama kweli tunautafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake.
🔘 *Kitu cha pekee kabisa tunachoweza kufanya ni kufikiri kwa makini na kwa wazi ikiwa tunatamani kuweka bidii inayohitajika ili kupata tumaini la Kikristo na kujipatia mbingu ya Kikristo. Ikiwa kwa neema ya Kristo tunaamua kufanya hivyo, swali linalofuata ni: Ni kitu gani nilicho nacho ninachopaswa kuondoa maishani mwangu ili kwamba nisijikwae?*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮♂️
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment