*Maana Bwana Mungu atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya.* Isaya 50:7
🔷 Umenunuliwa kwa gharama isiyo na kikomo nawe si mali yako mwenyewe. Nafsi, mwili, na moyo ni vya Yesu Kristo nawe unapaswa kwa unyenyekevu wote, lakini kwa uthabiti na uamuzi, kusema “mimi ni wa Bwana, nitatumikia kwa moyo, akili, uwezo na nguvu zangu zote.”
🔷 Usikatishwe tamaa kwa upinzani unaokutana nao. Inaweza kuwa inafurahisha kwa wakati wa sasa kuelea na mkondo kwa vile mteremko toka haki na utakatifu kwenda giza na uasi ni rahisi, wakati ambapo yeye atafutaye kuifikia pwani ya milele atapaswa kupambana dhidi ya upepo na mkondo wa bahari. Imani na dini ambayo haiweki bidii katika roho au ya kishujaa katika matendo, bali imeharibiwa kwa mikondo ya kidunia ndio dini pekee inayotamaniwa na kuheshimiwa na huthaminiwa na dunia kama ya kufaa...
🔷 Dharau na kejeli, zinazochangiwa toka katika daraja la watu wanaotweza kweli ya Mungu, ni ujalizo wa uadilifu wa Kikristo. Kama ungekuwa wa dunia, ungefurahia tabasamu lake, kujisifu kwake, na kushangilia kwake. Ikiwa Yesu Kristo yu ndani yako, tumaini la utukufu, hali yako ya kiroho itakemea kiburi na ubadhirifu wa dunia...
🔷 Upinzani ambao unakutana nao unaweza kuthibitika kuwa wa manufaa kwako kwa namna nyingi. Utajenga daraja la maadili ya Kikristo ambayo mara chache sana huchipuka katika njia ya mafanikio na mwanga wa jua. Imani, uvumilivu, ustahimilivu, msimamo wa kimbingu, tumaini linaloongezeka katika majaliwa ni matunda ambayo huchipua na kukua katikati ya mawingu ya giza, tufani, na dhoruba. Miti ya misitu ambayo husimama peke yake na kuwekwa wazi kwa upepo mkali na tufani na dhoruba haitang’olewa kwa upepo mkali, bali itasimika mizizi yake ndani sana na kutawanya matawi yake kila upande, na kupendeza sana na kuwa imara kama athari za kustahimili tufani na dhoruba.
🔷 Hii inaweza kuwa pia kwa upande wetu. Unaweza kunyimwa huruma na msaada wa kibinadamu na unaweza kuhisi kwamba tumaini lako pekee ni kuinua mikono yako kwa maombi kwa Mungu na kuuning’iniza moyo wako usio na msaada kwa Mwokozi wako. Msaada unaoletwa na mbingu utakuwa kile unachohitaji hasa...
🔘 *Kama unamcha Mungu, hupaswi kuogopa chochote pembeni. Ikiwa unampendeza, utajipatia kila kitu moyo wako unachohitaji.*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment