» » NJIA ZA MSAADA KATIKA UTUNZAJI SAHIHI WA SIKU YA BWANA


1.Siku ya BWANA huanza wakati wa jioni na kumalizika jioni wakati wa jua kuzama, hivyo basi, kupika, kusafisha nyumba, kufua, kunyoosha nguo, na kazi nyingine zote za kawaida zinatakiwa kuwa zimemalizwa kabla ya Siku ya BWANA kuanza. Kubadilika kwa siku usiku wa manane kulifanywa na warumi, lakini siku ya Mungu huanza jua linapozama hadi jua linapozama tena siku inayofuata, soma Zaidi kuhusiana na hili. Ifanye Sabato iwe siku ya pekee kwa kuandaa chakula malum, na vitu vya kufanya kwa ajili ya familia yako. Soma Zaidi na waulize wengine wakupe mawazo Zaidi isije ikawa wanatamani Sabati iishe ili “wajiachie”. Omba upate ufunuo toka kwa Mungu maana haiji kirahisi! Kama ambavyo unaweza kupanga shughuli nyingine za kifamilia kwa furaha, Siku ya BWANA inahitaji maandalizi na tafakari. Siku hii imeitwa Sabato katika Maandiko Matakatifu na katika lugha zaidi ya mia moja duniani.


2.Ni sahihi siku ya BWANA kupasha chakula chako ulichopika siku ya Ijumaa.


3.Ingekuwa vyema kujiepusha na vitabu vingine vyote vya kidunia, majarida, magazeti, mtandao wa internet, Iphone, Redio, vipindi vya televisheni ama mambo yote yahusikanayo na teknelojia, n.k mpaka Siku ya BWANA itakapoisha.

4.Miamala ya kibiashara kama Benki, malipo ya kodi, migahawa, kununua gesi, kununua magazeti, kuuza maziwa, vinywaji baridi n.k vinatakiwa kusubiri mpaka masaa ya Siku ya BWANA yameisha, ambayo humaanisha jioni ya Jumamosi baada ya jua kuzama. Jaribu “kutosimama langoni” kama walivyofanya kipindi cha Nehemia, wakisubiri Siku ya BWANA iishe ili kwamba wauze bidhaa zao. Kwa ufupi usikope siku moja ya Mungu, wakati ambapo amekupatia siku 6 kufanya kazi zako.


5.Sherehe, Mikusanyiko ya kijamii, na shughuli nyingine zote za kidunia kama mipira, kuogelea, Tennis n.k kamwe isingeruhusiwa katika Masaa matakatifu.



6.Siku ya BWANA mchana ni muda mzuri kwa vijana na watu wazima kushiriki katika kutembelea viumbe vya asili na kujifunza juu ya mimea na maisha ya wanyama. Si vyema kubadili muda wa ushirika wa kanisa na maburudisho ama kutembelea viumbe wa asili. Masaa ya Siku ya BWANA ni muda mzuri pia wa kutembelea wagonjwa waliofungwa na waliolazwa hospitalini. Kutembelea wagonjwa, wafiwa ama wafungwa wakati wa muda wa Ibada, inatakiwa kufanyika kwa nadra sana labda tu kama ni jambo la dharura ama tukio mahususi. Ni rahisi kupata uhuisho kwenye ushirika na wenzio na unaweza kujenga ushirika na watu hao baada ya hapo. Nadhani, mifano tuipatayo katika Biblia YESU hakuahirisha kwenda kusali kwasababu alikuwa anaenda kumuona mgonjwa. Aliendelea kufanya hivyo muda wote baada ya Ibada kanisani. Bila shaka “ hakukopa muda wa Kanisa”


7.Ni muda mzuri wa kujifunza mwongozo wako wa kujifunza Biblia kila juma siku ya BWANA mchana wewe na familia yako na kama ikiwezekana shiriki katika michezo ambayo itakuza mahusiano yako na Mungu (Michezo ya Biblia).


8.Mungu hufurahishwa tunapojitenga mbali si tu na kazi, lakini pia kujiepusha kuzungumza maneno yetu na kuwaza mawazo yetu siku ya BWANA. Hili ni gumu lakini omba kwamba ni jambo ambalo mafarisayo walikuwa na shida nalo, matendo yao yalikuwa sahihi, lakini dhamira, mawazo na tabia zao zilikuwa mbali mno. Najikuta mara kadhaa nikiwa nafuta koki za bafuni ama kuondoa utando wa buibui bila kufikiri kuwa ni sabato.


9.Tunaonesha dharau kwa Mungu, tunapoamua kulala masaa yote ya Sabato na kujitenga na Ibada katika nyumba ya Mungu ( japo si dhambi kupumzika saa moja ama mawili siku ya Sabato mchana, ila kulala siku nzima ili kwamba usome usiku, ama upate nguvu za kufanya mambo yako baada ya Siku ya BWANA si njia sahihi.


10.Tunamheshimu Mungu kwa kukusanya familia yetu pamoja, tukiimba kwa mtizamo wa Ibada wakati wa kufungua na kufunga Siku ya BWANA.



==========================================================


Kanuni zinazohusiana na MAMLAKA katika familia yetu…


1.Tunampenda na kumtii Bwana wetu, Mungu kwa unyenyekevu wa moyo wote

2.Tunasoma Biblia na kuomba kila jambo kwa Mungu kwa moyo mnyoofu

3.Tunawajali na kuwatii wazazi wetu katika Bwana bila kuonesha hali ya dharau

4.Tunakubali kukosolewa na  kuonywa kwa moyo wa unyenyekevu.


Kuhusiana na masuala ya MAHUSIANO katika familia yetu….

5.Tunapendana, kwa kuchukuliana kwa huruma, utu na staha

6.Tunasaidiana, kwa upole tunatanguliza mahitaji ya wenzetu kabla ya mahitaji yetu.

7.Tunatiana moyo, kwa kutumia maneno yale tu yanayojenga tabia njema na kubariki wengine.

8.Tunasameheana, kwa kufunika kosa kwa upendo pale tunapokosea ama kuwakosea wengine.


Kuhusiana na UMILIKI WA MALI katika familia yetu……


9.Tunashukuru Mungu kwa kile tulicho nacho, kwamba kiwe kidogo ama kingi.

10.Tunaridhika kwa kile tulicho nacho, na sio kutamani vingine wengine walivyo navyo.

11.Tu wakarimu kwa vile tulivyo navyo, kwa kushiriki kwa uwazi na wengine.

12.Tunajali vile tulivyo navyo, kwa kuvitumia kwa busara na kwa umakini.


Kuhusiana na KAZI katika familia yetu……


13.Tunabidii kukamilisha kazi kwa uaminifu na kwa umakini tunapoombwa kufanya hivyo.

14.Tunachukua juhudi binafsi kufanya kazi zetu zote pasipo kuhitaji kuambiwa

15.Tunafanya kazi kwa roho ya ushirikiano, kwa uwazi tunatoa na kupokea msaada.

16.Tunafanya juhudi binafsi kuhakikisha kuwa mazingira ya nyumbani yanadumu kuwa masafi muda wote.

Kuhusiana na TABIA katika familia yetu…..


17.Tunachagua kuwa na furaha, hata pale ambapo tunahhisi tulitakiwa kulalamika

18.Tunachagua kuwa wapatanishi, hata pale tunapojihisi kupisana kauli.

19.Tunaamua kuwa watulivu, hata pale tunapojihisi kama tunashindwa kutulia

20.Tunaamua kuwa wapole, hata kama tunahisi hatukutakiwa kuwa hivyo.

.

Kuhusiana na CHAGUZI katika maisha yetu…..


21.Tunafanya kile tunachojua kuwa ni sahihi, bila kujali wengine watasema nini.

22.Tunauliza kabla ya kutenda, pale ambapo hatujui nini sahihi cha kufanya

23.Tunajaribu kujizuia mar azote na kwa kila hali.

24.Daima tunasema ukweli na kamwe hatujaribu kusema uongo wa aina yeyote.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...