» » KESHA LA ASUBUHI Jumamosi 06/02/2021

MOYO WENYE SHUKRANI



*Na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.* Waefeso 5:20 


💎 Ingempendeza Bwana kama ungefanya juhudi katika kusahau mambo yako. Anza kumshukuru Mungu kwa ajili ya mji wako na mazingira yenye kuvutia, na baraka za maisha anazokupa. Kwa kurudisha shukrani kwa Bwana kwa ajili ya wema wake, unaweza kufanya jambo kwa ajili Yake yeye aliyefanya yote kwa ajili yako. Tafakari kina cha upendo na huruma ambazo Mwokozi amehisi kwa ajili yako. Kwa ajili yako alitoa maisha yake, akipitia kifo cha kikatili cha msalaba. Je, huwezi kumsifu Bwana kwa hili? Kama utayaficha maisha yako katika Kristo atakupokea. 


💎 Ikiwa utaonesha kuwa una imani itendayo kazi, kwa kujaribu kila siku kutendea kazi nguvu ya nia, fahamu zako zitatiwa nguvu. Ninalifahamu hili kwa uzoefu. Ninakumbuka kwa habari yangu mwenyewe namna fahamu zangu zilivyopata uwashawishi wa haraka kadiri nilivyojaribu kuzifanyia kazi. Je, utajaribu kusonga mbele, na kuwa mchangamfu katika roho? Weka tumaini kwa Yesu. Kuwa na imani kwake, na kuvutwa kirahisi mikononi mwake. Utapokea baraka kubwa kwa kufanya mabadiliko katika mazoea yako... 


💎 Kwa miezi kumi na moja baada ya kwenda Australia, niliugua ugonjwa wa baridi yabisi. Nisingeweza kunyanyua mguu wangu toka sakafuni pasipo kupata maumivu makali... Katika kipindi hicho cha miezi kumi na moja ya kuugua... sikukata tamaa. Mkono wangu wa kulia, kuanzia kwenye kiwiko kushuka, ulikuwa mzima, kwa hiyo nilitumia kalamu, na nikaandika kurasa elfu mbili na mia tano za karatasi za barua kwa ajili ya kuchapishwa. Katika kipindi hiki, nilikuwa na maumivu ya kutisha maishani mwangu... 


💎 Lakini kwa haya yote kuna upande wa kufurahisha. Mwokozi wangu alikuwa karibu kando yangu. Nilihisi uwepo wake mtakatifu moyoni mwangu, na nilijawa shukrani sana. Miezi hii ya mateso ilikuwa miezi ya furaha kuliko yote katika maisha yangu, kwa sababu ya ushirika wa Mwokozi wangu... Upendo wake uliujaza moyo wangu. Kipindi chote cha ugonjwa wangu, upendo wake, huruma zake, vilikuwa faraja yangu... 


🔘 *Mtazame Yesu, Mwokozi wako mwenye huruma na upendo. Ukimkabidhi Kristo moyo wako usio na msaada, ataleta furaha na amani moyoni mwako. Atakuwa taji yako ya furaha, thawabu yako kubwa sana.*


*TAFAKARI NJEMA SANA*👮‍♂️

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...