» » JE, KUNA KUOKOKA HAPA DUNIANI???

🤔🤔🤔🤔 

kati ya mada zenye utata mada ya *kuongoka na kuokoka* ni mada ambayo unamalumbano mengi. leo tutahitimisha kwa ufafanuzi wa hali ya juu na kama mtu hataelewa basi aulize.

Lakini pia kwa ufafanuzi zaidi kuhusu wokovu au njia ya uzima gusa link hii
👇👇👇
https://youtu.be/KMKjjh0Z12w
👆👆👆

kabla hatujaanza mada yetu. watu wengi sana wanashindwa kuyaelewa maneno yafuatayo;-
*1* wokovu
*2* kuokoa (okoa)
*3* kuokolewa
*4* mwokozi
*5*  kuongoka (ongoka)
*6* kuokoka

hivyo nitatolea ufafanuzi kwa kila neno katika lugha ya kiswahili na biblia inalitumiaje neno hilo

*1* WOKOVU
           ni hali njema iliyowekwa kwa mtu aliekatika upotevu ili aichague au aikatae. Muda mwingine wokovu ni msaada ambao mtu anapewa ili umsaidie atoke katika shida zake
      Luka 3:6 """wote wenye mwili watauona *wokovu* wa MUNGU""""
     Luka 19:8,9
    """Zakayo akasimana, akamwambia BWANA, tazama................ YESU akamwambia, leo *WOKOVU* umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa ibrahimu""" waweza soma pia mdo 4:12 mdo 7:23
      
        Hivyo wanadam wote leo tumepata neema ya wokovu bure kwa dam ya YESU hivyo ni hiali yako kuupokea au kuukataa

*2* KUOKOA (okoa)

Huu ni uwezo ambao anakuwa nao muokoaji (mtoaji katika shida) au waweza sema ni kitendo cha mwenye uwezo kumtoa asie jiweza katika shida zake

Mthayo 18:11 """kwa kuwa mwana wa adam alikuja kukiokoa kilicho potea""""
  Hivyo wanadam asie jiweza katika dhambi alikuja anae weza kuzishinda dhambi na kumtoa mdhambi katika dhambi

      *3* OKOLEWA
Hii ni kitendo cha mwenye hali mbaya kukubali kutolewa katika hali yake mbaya 

 Hata kama ulimpokea YESU mwanzoni lakini ulianguka dhambini hivyo ukitubu unaokolewa tena katika hukumu ya dhambi hiyo

2 koritho 2:15 ""kwa kuwa sisi tu manukato ya kristo, mbele za MUNGU, katika wao *wanaookolewa* na katika wao wanaopotea""
 
*4* MWOKOZI
 
Huyu ni yule ambae anamtoa mtu asiejiweza au kitu kisicho jiweza katika katika hali mbaya na kukiweka katika hali nzuri.
      Luka 1:47 """Na roho yangu imemfurahia MUNGU *mwokozi* wangu"""
      Luka 2:11 ""maana leo katika mji wa daudi amezaliwa, kwa ajili yetu, MWOKOZI, ndiye KRISTO BWANA"""

*5* KUONGOKA 
     Hii ni hali ya mtu binafsi kukubali kutolewa katika hali mbaya au katika dhambi na kuanza kutenda mema Lakini mtu huyu anaweza kuahilisha kutenda mema na kurudia kutenda dhambi tena. Akirudia dhambi zake anakuwa hajaongoka maana mwanadam asili yake ni dhambi hivyo akirudia dhambi anakuwa bado haja badilika 
       Mathayo 18:3 ""akasema, amin, nawaambia, *MSIPOONGOKA* na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni""
        Yohana 12:40
""""Amewapofusha macho, ameifanya mizito mioyo yao, wasije wakaona kwa macho yao, wakafaham kwa mioyo yao, *wakaongoka*, nikawaponya"""

Hivyo mwanadam mwenye asili ya dhambi anapogeuka na kuacha dhambi katika dunia hii anaongoka lakini anaweza kuanguka tena katika dhambi kwani 
        1 yohana 2:1 ""watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi, *na kama mtu akitenda dhambi* tunaye mwombezi kwa BABA, YESU KRISTO mwenye haki""
    Kwa hiyo hapa duniani tunaweza kutenda dhambi lakini tukitudu katika uongofu (kudumu katika kweli ya MUNGU) basi tutatolewa katika dunia hii na tusijetenda dhambi tena na haiwezekani kutenda dhambi tena hapo tutaokoka na maovu ya dunia hii

*6* KUOKOKA 
      Ni hali ya kutolewa katika hali mbaya na kuwekwa katika hali njema ambayo hali hiyo haiwezekani kurudia katika hali mbaya. 
      Kwa mfano watu walio pata ajali ya meli wakabaki wanaogelea juu ya bahari au ziwa watu hao walio wazima katika bahari wanakuwa wameongoka kwani kuna uwezekano wa kufa au kupona ila wakitolewa katika hiyo bahari basi wanakuwa wameokoka na ajali ya meli hiyo. 

Mfano mwingine ni wa mdo 27,28 ambapo watu walipata dhoruba bahalini na paulo akawaambia wote tutaokoka lakini akawaambia kuwa mtu yoyote atakaye jilusha nje ya merikebu huyu hata okoka. Hivyo baada ya kutoka katika dhoruba ile ndipo wakasema mdo 28:1 """tulipokwisha *kuokoka* ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile kinaitwa melita""

Kwani walipo kuwa katika dhoruba ya bahari hawakukijua kisiwa kile mdo 27:39 ""kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha marikebu huko, kama ikiwezekana""

Baada ya kutoka katika dhoruba ile basi waliita kuokoka maana hawataweza kuirudia tena ile dhoruba 


Vivyo hivyo watu wa MUNGU wakivumilia katika uongofu. Wakidumu katika pendo la kristo YESU na wakivumilia shida na mateso wanayoyapata kwa ajili ya kulitetea jina la YESU basi mwisho YESU atakapo rudi atamtoa katika shida na dhiki za ulimwengu huu na hatarudia katika dhambi wala mateso ya dunia hii.
     Mathayo 24:21,22 kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe na kama siku hizo zisingalifupizwa *asingeokoka* mtu yeyote, lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
       Hivyo siku za dhiki zinakuja kwa watu wa MUNGU ambayo dhiki hiyo ya kukataa kutiwa chapa ya mnyama *666* ambayo wengi watauwawa na kuteswa sana lakini wakivumilia katika kweli ya MUNGU Basi YESU mwenyewe atashuka kuwakomboa watu wake. 

*MUNGU akubariki sana lakini pia waweza sabaza somo hili kwa wengine* 🙏🙏🙏🙏🙏

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...