» » KESHA LA ASUBUHI

ALHAMISI, FEBRUARI, 18, 2021
SOMO: MBINGU HUANZIA HAPA 

Jinsi zilivyo nyingi Fadhili zako, Ulizowawekea wakuchao: Ulizowatendea wakukimbiliao, Mbele ya wanadamu. 

Zaburi 31:19. 



Ninapoandika nina hisia za ndani za shukrani kwa ajili uangalizi wa upendo wa Mwokozi wetu juu ya wote. Ninaposoma Neno la Mungu na kupiga magoti katika maombi, ninavutwa na wema na rehema za Mungu kiasi kwamba siwezi kutoa maombi yangu pasipo kulia. Moyo wangu unazidiwa na kuvunjika ninapotafakari juu ya wema na upendo wa Baba yangu wa mbinguni. Nina njaa na kiu zaidi na zaidi kwa ajili ya Yesu katika maisha haya. Kristo alisulubiwa kwa ajili yangu, na je, nitalalamika ikiwa nitasulubiwa pamoja na Kristo ?



Sijawahi kuhisi shauku ya dhati kwa ajili ya haki kuliko wakati huu wa sasa. Katika saa ya kuamka ya usiku ombi langu ni, “Bwana, wafundishe watu wako jinsi ya kutafuta na kuokoa kondoo waliopotea.” 



Hatujui kile kilicho mbele yetu, na usalama wetu pekee ni kutembea na Kristo, mkono wetu katika wake, mioyo yetu ikijawa na tumaini kamilifu. Je, hakusema, “Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami” (Isaya 27:5)? Hebu na tusogee karibu na Mwokozi. Tutembee naye kwa unyenyekevu, tujazwe na upole wake. Hebu nafsi na ifichwe pamoja naye katika Mungu.... 



Moyo wangu huuma ninapooneshwa jinsi wengi wanavyofanya nafsi kuwa sanamu yao. Kristo amelipia gharama ya ukombozi kwa ajili yao. Anastahili utumishi wa nguvu zao zote. Bali mioyo yao imejawa kujipenda wenyewe, na tamaa kwa ajili ya kujipamba wenyewe. Hawatafakari kabisa juu ya maneno, “Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba, anifuate” (Marko 8:34). 



Miongoni mwa wale ambao watapatwa na uzoefu wa uchungu mkuu wa kukatisha tamaa siku ya kutoa hesabu ya mwisho, watakuwa wale ambao wamekuwa na dini ya mwonekano wa nje, na wale ambao walionekana kama wanaishi maisha ya Kikristo. Lakini ubinafsi umefungamana katika kila wanachofanya. Wanajivuna wenyewe juu ya uadilifu wao, mvuto wao, uwezo wao wa kusimama katika nafasi za juu kuliko wengine, na ufahamu wao wa kweli, kwa kuwa wanafikiri kwamba haya yatawafanya wapate kutambuliwa na Kristo. “Ndipo watakapoanza kusema, tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu” (Luka 13:26). “Hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?” (Mathayo 7:22).

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...