» » » » Utoaji ni nini? Zaka na Sadaka humfanya mtoaji kuwa Tajiri


Moja ya changamoto zinazolikabili kanisa ni kushuka kwa kiwango cha utoaji miongoni mwa waumini. Takwimu zinaonyesha kuwa watoaji wa michango, zaka na sadaka makanisani ni wastani wa asilimia 25 hadi 30 ya washiriki wote. Ni nini sababu ya hali hii na nini kifanyike kubadilisha sura hii inayoonyesha upungufu mkubwa wa Roho ya ukarimu miongoni mwetu? Haya ni baadhi ya mambo tutakayoyajadili katika kona hii, kwa kuleta mada mbalimbali za kujadiliana. Kwa kuanzia leo tutajadili mada ya utoaji na makundi mbalimbali ya watoaji. Karibu.

Utoaji ni nini?
Kutoa ni kushiriki na wengine kile tulichonacho na vile tulivyo. Kuna aina tano za watoaji:
  1. Baadhi ya watoaji ni kama kipande cha jiwe: Ni wagumu waliojifungia kwenye nafsi zao na wa baridi kama jiwe. Hawawezi kutoa kwa hiari yao wenyewe; wanatoa tu wanapolazimishwa kwa nguvu, na hata hapo watatoa kwa kinyongo na huku wakiwa cheche za hasira.

  1. Watoaji wengine ni kama dodoki: Dodoki hutoa maji pale tu linapokamuliwa. Likiwa lenyewe bila kuguswa haliwezi kutoa maji. Ni lazima lihimizwe na kutiwa moyo ndipo linaweza kutoa maji bila kinyongo na bado linajibakizia kiasi fulani cha maji.

  1. Watoaji wengine ni kama Mwembe:
Mwembe hutoa matunda kwa yeyote anayeutunza. Mwembe ni mkarimu. Hutoa matunda yake kwa rafiki na adui. Hudumu kutoa yote iliyonayo hadi yanapokuwa yamekwisha mtini.

  1. Watoaji wengine ni kama chemichemi inayobubujika:
Huendelea kububujisha usiku na mchana,ikiendelea kutoa bure maji yake mazuri na yenye kumetameta kwa wote. Haikomi kutoa. Haijali ikiwa watu wanayatumia maji yake au la, bado inaendelea kutoa. Utoaji wake haukomi. Kutoa ni sehemu ya maisha yake.

  1. Bado watoaji wengine ni kama sega la asali:
Sega la asali halitoi tu kile ilichonacho, bali huwajaza inaowapatia utamu na furaha. The honeycomb not only gives what he has, but it fills those who share of her, with sweetness and delight. Huwakamulia watu wema, utamu na furaha.

MASWALI YA KUJADILI:
  1. Nini maana ya kutoa?
  2. Nini maana ya kushiriki na wengine?
  3. Kuna tofauti yoyote baina ya “kutoa” na “kushiriki na wengine”? Fafanua.
  4. Kuna tofauti gani baina ya “kutoa” kile mtu alichonacho na vile alivyo?
  5. unakubalianan na aina tano mbalimbali za watoaji zilioelezwa hapo juu? Unaweza kutaja aina zingine zaidi za watoaji? Hebu zitaje.
  6. Chambua sifa za mtoaji aliye mithili ya:
  • Jiwe
  • Dodoki
  • Mwembe
  • Sega la asali.
  1. Katika uzoefu wako, umewahi kukutana na watu wanaoelezwa na aina hizo mbalimbali za watoaji? Toa mifano.
  2. Wewe ni mtoaji wa aina gani? Ni nini kinachokufanya kusema hivyo?
  3. Tafuta katika Injili watu walio kwenye makundi hayo ya watoaji. Yesu alikuwa mtoaji wa kundi gani? Eleza

Hatutakiwi kuwa mitungi ya kuhifadhia upendo bali mifereji inayobubujisha upendo.
Toa hadi unasikia maumivu. Usitoe mazidio yako tu toa hata na vile vilivyosalia.

MAFUNGU YA Biblia YANAYOZUNGUMZIA UTOAJI
Mathayo 2:9-11 Mamajusi wakitoa zawadi zao bora mno kwa Yesu
Mathayo 5:28-42 Kuhusu kulipiza kisasi. Wapatie adui zako kwa upendo.
Mathayo 6:1-4 Namna ya kutoa kwa upendo na kwa faragha
Mathayo 7:1-6 Katika kuhukumu wengine. Mungu atatumia kipimo hicho hicho kwako
Mathayo 7:12 Watendee wengine kam ambavyo ungependa wao wakutendee wewe
Mathayo 10:5-10 Utume wa Mitume 12. Toeni bure.
Mathayo 10:40-42 Zawadi kwa watoaji
Mathayo 12:33-35 Utautambua mti kwa matunda utoayo
Mathayo 14:13-21 Kulisha watu 5,000. Alitoa vyote alivyo navyo
Mathayo 18:21-35 Toa na kusamehe madeni yako. Mtumishi asiyesamehe.
Mathayo 26:26-29 Chakula cha mwisho. Yesu ajitoa mwenyewe kwenye Meza ya Bwana
Mako 10:26-29 Kijana Tajiri ashindwa kutoa…
Mako 12:41-44 Mjane aliyetoa vyote alivyonavyo.
Luka 3:10-14 Mafundisho ya Yohana mbatizaji.
Luka 5:27-28 Wito wa Mathayo. Atoa vyote.
Luka 6:38 Mungu atatupima kwa kipimo kile kile tunachopimia wengine.
Luka 12:13-21 Kisa cha Tajiri mpumbavu. Alipoteza kila kitu.
Luka 12:32-34 Utajiri mbinguni. Toa yote uliyonayo duniani.
Luka 16:19-31 Kisa cha Tajiri na Lazaro.
Luka 19:1-10 Zakayo atoa nusu ya mali yake.
Matendo 2:43-47 Maisha ya wakristo wa awali. Kushirikiana vyote walivyonavyo.
Matendo 5:1-13 Anania na Safira. Waliadhibiwa kwa uchoyo wao.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...