» » » » IKULU YA MAREKANI ILIVYOMKABIDHI ANNA HENGA MKURUGENZI WA LHRC TANZANIA TUZO YA UJASIRI (+VIDEO)



Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga, akionyesha Tuzo ya Kimataifa ya Mwanamke Jasiri kwa mwaka 2019 baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo (kushoto) na Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump Machi 7 mwaka huu jijini Washington D.C.( Picha/Video na Ubalozi wa Marekani )


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Anna Henga amekuwa miongoni mwa  wanawake 10 waliotunukiwa Tuzo ya Mwanamke Jasiri (mwenye uthubutu) Duniani (International Women of Courage Award), 2019, tuzo inayoandaliwa na Ikulu ya Marekani chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, Mike Pompeo ambaye ndiye aliyekabidhi tuzo hiyo akiwa na Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump.

Tuzo hiyo ilitolewa Machi 7,mwaka huu katika Ikulu ya Marekani na tukio hilo lilioneshwa mbashara kupitia twitter,Facebook na Tovuti ya  Ikulu ya Marekani 
Bi. Anna Henga alitajwa kuwa ni moja ya wanawake waliotunukiwa tuzo hiyo kufuatia juhudi zake katika utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania hasa kwa upande wa jamii ya kimaasai. 

Wanawake wengine tisa waliotunukiwa tuzo hiyo wanatoka katika nchi za  Egypt, Jordan, Ireland,Bangladesh, Burma, Djibouti,Montenegro, Peru na Sri Lanka.

D.C. Anna Henga anakuwa ni Mtanzania wa pili kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Mwanamke Jasiri, akifuata nyayo za Vicky Ntetema aliyepata tuzo hii mwaka 2016 

Tuzo ya International Women of Courage ilianzishwa mwaka 2007 ili kutambua mchango wa wanawake wanaojitoa kwa nguvu na ujasiri kama viongozi katika kuleta mabadiliko chanya kwenye  jamii zao bila kujali hatari ya maisha yao binafsi. 

Mpaka sasa, kupitia tuzo hiyo Ikulu ya Marekani imetambua mchango wa wanawake zaidi ya 120 kutoka nchi zaidi ya 65 katika kutetea haki za binadamu, kudumisha nafasi ya wanawake katika jamii, amani na utawala bora katika nchi zao.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...