» » Mkutano mkubwa wa Chama cha Wanataaluma wajasiriamali wa Kanisa la Wadventista Wasabato Tanzania (ATAPE)





Mkutano mkubwa wa Chama cha Wanataaluma wajasiriamali
wa Kanisa la Wadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), umeanza rasmi leo mkoani
Simiyu.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umebainisha
mafanikio yaliyofikiwa na chama hicho ikiwamo kupata zaidi ya Sh bilioni moja
katika miradi ya maendeleo nchini.
Mkutano huo unaofanyikia katika Shule ya Sekondari
Kusekwa iliyoko Mjini Bariadi, zaidi ya wanataaluma na wajasiriamali 1,500
kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wameshiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa
chama hicho, Freddie Maneto amesema ATAPE kimewekeza katika miradi ya Afya,
Kilimo, Elimu, Maji, pamoja na ujasiriamali.
“Tuna hospitali mbalimbali, shule, mashamba
zaidi ya hekari 10,000 ambayo tumelima mihogo, miti na korosho, hivyo tunapoadhimisha
miaka 20 ya uwepo wa chama chetu, tunajivunia kuwa miongoni mwa taasisi ambayo
imeajiri Watanzania wengi,” amesema Maneto.
Aidha, mwenyekiti huyo amesema katika kutoa
huduma kwa wananchi, wanatarajia kuleta mradi wa maji mkoani Simiyu, kutokana
na mkoa huo kuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi wake.
Hata hivyo, wananchi wa mkoani Simiyu
wameushukuru uongozi wa mkoa kwa kuendelea kuwaletea fursa mbalimbali ambapo
wanategemea kuongeza kipato kupitia biashara zao.
“Hii ni fursa kubwa kwetu, kama wananchi wa
Simiyu, watu zaidi ya 15,000 ni wengi tutaongeza kipato kupitia biashara
mbalimbali, kwa sasa katika mji wetu wa Bariadi nyumba za kulala wageni zote
zimejaa, watu wamefanya biashara,” amesema John Bubinza mkazi wa Bariadi.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...