» » RC MTAKA AWASIHI WATANZANIA KUTUMIA FURSA YA KUWEKEZA MKOANI SIMIYU

RC MTAKA AWASIHI WATANZANIA KUTUMIA FURSA YA KUWEKEZA MKOANI SIMIYU


RC MTAKA AWASIHI WATANZANIA KUTUMIA FURSA YA KUWEKEZA MKOANI SIMIYU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Mhe. Anthony Mtaka akisisitiza jambo wakati akifungua Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu.   Mkuu wa Mkoa ...
 MHE BITEKO AANZA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUKOMESHA UTORO MASHULENI, ACHANGIA MATOFALI 10,000 UJENZI WA MAABARA
 WANAMABADILIKO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME
 KAMPUNI YA IVORI IRINGA YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA TOSAMAGANGA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Mhe. Anthony Mtaka akisisitiza jambo wakati akifungua Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Anthony Mtaka (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel (kushoto), na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper, Dkt Jim Yonazi (kulia) wakisikiliza maelezo mbalimbali katika Kongamano hilo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisisitiza umuhimu wa Viwanda nchini Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate Bank Ltd, Bi Theresia Soka (kulia) akiwa na Zacharia Kicharo Meneja wa TIB Development Bank Ltd Lake Zone wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg Jumanne Sagini akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Anthony Mtaka kuzungumza na wafanyabiashara na wawekezaji waliojitokeza katika kongamano la uwekezaji.
Kutoka Kulia ni Emmanuely Gungu Silanga Mwenyekiti wa Viwanda Mkoa wa Simiyu, Peter Bahini Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato (ATAPE) Kanda ya Nyanza Kusini (SNC) na Emmanuely Lupembe Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato (ATAPE) Kanda ya Nyanza Kusini (SNC wakifatilia kwa makini kongamano la uwekezaji Mkoani Simiyu.



Meza kuu wakifatilia mjadala katika Kongamano la Jukwaa la Biashara Simiyu
Kwaya ya AIC Bariadi, Simiyu wakiimba wimbo maalumu kwa ajili ya kuhamasisha ulipaji kodi
Washiriki wa kongamano la Jukwaa la Biashara
Mkurugenzi wa METDO Tanzania Bw Ashraph Omary (Kulia) akifatilia kwa makini Kongamano hilo
 Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper Dkt Jim Yonazi  akisisitiza akielezea dhamira ya TSN kuamua kufanya kongamano hilo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoani Simiyu akitoa salamu zake za pongezi kwa ufanikishaji wa kongamano hilo
Katikati ni Emmanuely Gungu Silanga Mwenyekiti wa Viwanda Mkoa wa Simiyu akifuatilia kwa makini Kongamano
Wafanyakazi wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka
Kutoka Kulia ni Mtafiti Mwandamizi (TSN) Bw Akim Joseph, Afisa masoko Mwandamizi (TSN) Goodluck Chuwa, Mwakilishi wa TSN Kanda ya ziiwa Patrice Simbachawene na Meneja wa Masoko na Mauzo wa TSN Bw Januarius Maganga
Mbunge wa Busega Mkoani Simiyu Mhe Raphael Chegeni akitoa salamu za shukrani kwa kufanikiwa kwa kongamano hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel (kushoto), na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper Dkt Jim Yonazi (kulia) wakiteta jambo wakati wa Kongamano
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate Bank Ltd Bi Theresia Soka akiwasilisha Mada
Mhariri Mtendaji wa www.wazo-huru.blogspot.com Ndg Mathias Canal akiendelea na kazi ya kuhabarisha kuhusu kongamano hilo
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw Richard Kayombo akielezea namna ya ukusanyaji Mapato
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na wadau wawezeshaji wa Kongamano hilo
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji Mkoani Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Anthony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Anthony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na Waimbaji wa Kwaya ya AIC Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Anthony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshiriki kuhabarisha kuhusu Kongamano hilo.


Na Mathias Canal, Simiyu


Wafanyabiashara na wadau wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kutumia fursa za uwekezaji wa biashara hususani katika kuwekeza kwenye viwanda kwani mipango mingi inayopangwa na serikali inatoa fursa zaidi kwa wawekezaji wa ndani ya nchi jambo ambalo litaifanya Tanzania kuondokana na umasikini kutokana na fursa zilizopo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka wakati akifungua Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu lililofanyika katika Ukumbi wa Parokia ya Mtakatifu John lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.

Rc Mtaka amesema kuwa Katika kuchochea na kuleta maendeleo  kwa wananchi katika Mkoa wa Simiyu uongozi wa Mkoa huo una dhamira ya dhati kuwafanya wananchi wake kuingia katika ramani ya Mkoa unaotumainiwa nchini.

“Sisi viongozi kwa kushirikiana na wananchi tunapaswa kutumia Busara nyingi, Hekima na Utii ili kuimarisha utendaji katika maendeleo ya Mkoa kwa kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo pasina kutumia majungu ambayo yatadhoofisha maendeleo” Alisisitiza Mhe Mtaka

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel amewasihi wananachi ambao ni wafanyabiashara na wawekezaji katika Mkoa wa Simiyu na wale wanaotaka kuwekeza Mkoani humo kufanya biashara na kuhakikisha wanalipa kodi kwa mujibu wa sheria kwani wasipofanya hivyo biashara zao haziwezi kuwa na maendeleo kwani watakuwa wameenda kinyume na mamlaka ya Mungu inayoagiza kulipa kodi.

Profesa Gabriel amebainisha hayo huku akihuisha na maneno yaliyoandikwa katika Biblia Takatifu kwenye Kitabu cha Warumi 13:1-7 ambayo inaeleza vyema kwamba Mtu wa kodi apewe kodi na Mtu wa Ushuru apewe ushuru hivyo wafanyabiashara hao wanapaswa kutii mamlaka iliyo kuu kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.

Amesema Uongozi wa Mkoa wa Simiyu kupitia Mkuu wa Mkoa huo kuwa wanapaswa kuendelea zaidi kuwa wabunifu katika shughuli mbalimbali ili Simiyu iendelee kukua zaidi katika uwekezaji na maendeleo.

Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper inayochapisha magazeti ya Habari Leo, Daily News na Sport Leo Dkt Jim Yonazi amesema kuwa kampuni hiyo ya TSN imeamua kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ili kuufanya mkoa huo kuungana na Dunia katika kuakisi uwekezaji hususani katika sekta ya Viwanda.

Dkt Yonazi amesema kuwa kampuni ya TSN ina amini kuwa maendeleo ni habari hivyo kupitia Jukwaa hilo la Biashara katika Mkoa wa Simiyu watanzania na Dunia kwa ujumla itafahamu vyema juu ya umuhimu wa uwekezaji hivyo kupitia umoja na mshikamano kwa wafanyabiashara na wawekezaji katika Mkoa huo utakuwa chachu ya mafanikio ya Tanzania nzima.

Hata hivyo amesema kuwa Mkutano huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya nguvu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo hata hivyo amewasihi wawekezaji na wadau wa Maendeleo kutumia nguvu hiyo kwa ajili ya biashara zao.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw Richard Kayombo ameelezea sababu za wawekezaji na wananchi kulipa kodi ambapo amesema kuwa njia pekee ya ambayo serikali inaweza kujipatia kipato chake kwa ajili ya kuwajengea wananchi Miundombinu bora, Kudumisha sekta ya Afya, Elimu na sekta zingine nyingi ni kukusanya kodi pekee.

Hata hivyo alisema kuwa zipo sekta ambazo kisheria zinapewa msamaha wa kutokulipa kodi ambapo ni pamoja na sekta ya Kilimo sambamba na sekta ya elimu na afya.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate Bank Ltd Bi Theresia Soka amesema kuwa Bank hiyo ni maalumu kwa ajili ya shughuli za maendeleo na Biashara hivyo wajibu wake ni kufanya kazi ili kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi hususani katika msaada wa kifedha.

Wadau wengine walioshiriki katika Jukwaa hilo la Biashara ni pamoja na TIB Development Bank, National Microfinance Bank (NMB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na TIB Development Bank Ltd.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...