» » » » UTEKELEZAJI WA UTUME WETU KIWIRA

Karibuni kwenye tovuti ya Kanisa la Waadventista Wasabato Kiwira ili ujipatie maarifa mengi ya kukuimarisha kiroho, kiakili, kimwili, na kijamii. Hapa utakutana na Yesu atakayebadilisha maisha yako ya sasa na ya umilele. Karibu ushiriki nasi. TAMKO LA UTUME UTUME WETU: Utume wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kiwira, ni kuwafanya watu wote wawe wanafunzi kwa kuwapelekea Injili ya milele iliyo katika muktadha wa Ujumbe wa Malaika Watatu wa Ufunuo 14:6-12, kuwaongoza wampokee Yesu kama Mwokozi wao binafsi, na kuwaita kujiunga katika Kanisa lake la Masalio, wakifundishwa kumtumikia Yeye kama Bwana wao na kuwaandaa kwa Marejeo yake yaliyo karibu. UTEKELEZAJI WA UTUME WETU: Tunatekeleza Utume wetu chini ya uongozi na uwezeshaji wa Roho Mtakatifu kwa kufanya yafuatayo: Kuhubiri – Kwa kulikubali agizo la Kristo la Mathayo 28:18-20, katika siku hizi za mwisho, tunautangazia Ulimwengu wote Injili ya Milele ya Upendo wa Mungu, anayefunuliwa wazi kupitia maisha , utume, kifo, ufufuo na huduma ya ukuhani wa mwanaye Yesu Kristo. Kwa kutambua kwamba Biblia ni kitabu cha Mungu kisichoweza kukosolewa, kinachofunua mapenzi ya Mungu, tunaueleza ukweli wote wa Biblia, ukiwemo ule wa kuja kwa Kristo mara ya pili na mamlaka endelevu ya Amri Kumi za Mungu, zenye ujumbe wa kutukumbusha kuitakasa siku ya saba ya juma kama Sabato. Kufundisha – Tukikiri kwamba maendeleo ya mwili na tabia ni vya muhimu katika mpango wa Mungu wa Ukombozi, tunahimiza ukuaji katika kumwelewa Mungu na jinsi ya kuhusiana na Yeye, na Neno lake, pamoja na vitu vyote alivyoviumba. Uponyaji – Kwa kuzithibitisha kanuni za Biblia za kuwa na utu wote mkamilifu, tunafanya utunzaji wa afya zetu na uponyaji wa wagonjwa kuwa kipaumbele chetu. Kwa kuwahudumia maskini na wanaoteseka, tunashirikiana na Muumba katika kazi yake ya urejeshwaji kwa njia ya matendo ya huruma. Kufanya wanafunzi – Kwa kuthibitisha ukuaji wa kiroho ulio endelevu kwa maendeleo ya waumini, tunatoa malezi kwa waumini wapya, tukiwafunza kuishi maisha ya haki na kuwaelekeza kushuhudia kwa mguso wenye nguvu na kuwatia shime kuonyesha mwitikio wa utii kwa mapenzi ya Mungu. NJOZI YA UTUME WETU: Kwa kupatana na unabii unavyofunuliwa katika Maandiko, tunauona utume wetu ukifikia kilele katika Mpango wa Mungu wa urejeshwaji wa viumbe vyake katika ukamilifu wa mapenzi yake na haki yake.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...