» » RC Gambo Atoa Neno la Faraja kwa Vijana

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kuwatia moyo vijana waache tabia ya kuishi katika maisha ya kulia kila siku bali wanapaswa waishi kwa furaha ili waweze kupata baraka za Mungu.

Mrisho Gambo amesema kupitia ukurasa wake maalum wa Facebook baada ya kuwepo na desturi ya watu wengi kuwa na uoga wa maisha huku wengine wakiogopa kusema mbele za watu kwamba huwa wanalia kutokana na kukosa jambo fulani katika maisha yao.

"Usiishi maisha ya kulia kila siku, lazima ifike kipindi useme sasa kulia basi. Kulia kwa uchungu sio maisha, maisha ni kulia kwa furaha, wengi wanaona aibu kusema wamelia sana, mimi nitakuambia ukweli ninalia sana lakini ninamlilia Mungu simlilii binadamu", amesema Mrisho.

Pamoja na hayo, Mrisho ameendelea kwa kusema "Anza kulia na Mungu wako, wanaokucheka waache uchungu ni wao, lia kwa ajili ya watoto wako. Mlilie Mungu kwa ajili ya wazazi, kazi na biashara yako, Mungu akikufuta machozi utaona baraka hata kwa watoto wako, wazazi, kazi hata biashara yako", amesisitiza Mrisho.


Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles