Mwanamke asiyekuwa na upendo kwa ndugu wa mume wake tazama mumewe alichomfanyia................
Siku moja wakiwa wamekaa pmj mume pmj na mke wake mume akamwambia mke wake
"Mke wng nimewakumbuka sana ndugu zng (kaka zng dada zng na ata baba na mama) tujumuike pmj na kula pmj,,,,
Kesho nitawaalika ili tujumuike nao ktk chakula cha mchana,itabidi uandae chakula kwa ajili yao."
Mke akasema kwa unyonge "Sawa mungu akipenda."
Asubuhi ya siku iliyofuata mume akatoka kwenda ktk mishughuliko yake lkn baada ya masaa kadhaa akarejea nymbn na kumuuliza mke wake.
"Mke wng umeandaa chakula cha mchana kwa ajili ya wageni? maana baada ya lisaa limoja watakuwa wameshafika."
Mke akajibu "hapana sijapika kwani ndugu zako sio wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."
Mumewe akamwambia "m/mungu akusamehe mke wng kwa nn unayasema hayo ilihali tokea jana nilikuambia ya kuwa wazazi wng wanakuja
Na kwa nn hukuniambia mapema kuwa hutopika ilihali baada ya lisaa limoja wazazi wng watakuwa hapa nn unafanya mke wng."
Mke akamjibu "waache waaje nitawataka radhi kwani wao si wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."
Basi mume ikambidi aondoke pale nymbn kwa kukwepa fedheha.
Baada ya dakika kadhaa mlango ukagongwa mke akaenda kuufungua.
Kwa mshangao mkubwa alipofungua mlango akakuta wageni waliokuja hapo ni wazazi wake babaake mamaake dada zake pmj na kaka zake.
Akastuka kwa mshangao na kuwakaribisha ndani,
Baba akamuuliza kuwa mume wake yupo wapi?
Akajibu yule mwanamke kuwa alikuwepo hapa ametoka dakika chache kabla hamjafika.
Baba akamwambia "mumeo jana alitupa taarifa kuwa Leo anatuarika hapa tuje kula pmj chakula cha mchana sasa vipi yy ametoka si busara."
Yule mwanamke akastuka kwa taarifa hiyo na kuanza kujifikicha mikono yake huku akiipiga piga hali ya kuchanganyikiwa."
Ikambidi aingie ndani na kumpigia simu mume wake akamwambia "kwa nn hukuniambia kuwa wazazi wng ndio wanaokuja?"
Mumewe akamjibu "Wazazi wng na wazazi wako wote ni kitu kimoja/hawana tofauti."
Mke akamwambia "Lete chakula huku chakula kilichokuwepo ni kichache haki tawatosheleza."
Mume akamjibu "Mm nipo mbali na hao si wageni watakula chochote kilichopo kama ww ulivyokuwa ukitaka kuwalisha wazazi wng.
Hili liwe ni somo kwako juu ya kuwaheshimu wazazi wng."
Watendee watu kama vile unavyopenda kutendewa ww

No comments:
Post a Comment