» » Mawakili Watimuliwa Nchini

Serikali ya nchini Tanzania imewafukuza mawakili watatu wa Afrika Kusini waliokamatwa wiki hii Jijini Dar es Salaam wakituhumiwa kwa kuchochea mapenzi ya jinsia moja.

Mawakili hao waliofukuzwa ni wale waliokuwa miongoni mwa watu 13 waliokamatwa katika hoteli moja mjini Dar es Salaam wakijiandaa kufanya mkutano wa kujadili iwapo wakabiliane na uamuzi wa serikali ya Tanzania kuzuia utoaji wa baadhi ya huduma za afya au la kwa mujibu wa mawakili hao.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa jana wakati akizungumza na wanahabari  amewaambia kuwa kabla ya mawakili hao kukamatwa walikuwa wakichochea mapenzi ya jinsia moja.

Mapema mwaka huu, serikali ilipiga marufuku baadhi ya kliniki za kibinafsi kutotoa huduma za ugonjwa wa HIV na ukimwi ikisema zilikuwa zikukuza mapenzi ya jinsia moja ambayo ni haramu nchini Tanzania.

Hata hivyo kukamatwa kwa Mawakili hao kunatokea kufuatia hotuba ya mwezi Septemba iliotolewa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis Kingwangala (kwa sasa ni Waziri wa Maliasili) ambaye aliapa mbele ya bunge kukabiliana na makundi yoyote yanayounga mkono wapenzi wa jinsia moja nchini.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...