» » Watu 11 Wakamatwa Wakiandamana Kupinga Tundu Lissu Kupigwa Risasi

Watu 11 wakiwemo madiwani wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya IKungi mkoani Singida wamekamatwa wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kuishinikiza Serikali kutoa tamko kuhusu kuvamiwa na kupigwa risasi mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu amesema watu hao wamekamatwa na polisi juzi Ijumaa mchana wakiwa na mabango katikati ya mji wa Ikungi, wakiwa kwenye harakati za kuhamasisha maandamano.
“Walitaka kufanya maandamano, tuliwawahi kabla hawajaanza, miongoni mwao wapo waliotokea Arusha na Dodoma, kwa hiyo wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi," amesema Mtaturu.

Amesema tukio la Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kupigwa risasi halijatokea Singida, hivyo hawataruhusu maandamano ya aina yoyote yanayoweza kuhatarisha amani.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...