» » Gwajima Kumuomea Tundu Lissu

Mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima  wa kanisa la Ufufuo na Uzima amefunguka na kusema kuwa siku ya Jumapili atafanya maombezi maalum kwa afya ya Mbunge Tundu Lissu ambaye juzi alipigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Dodoma nyumbani kwake.

Mchungaji Gwajima amesema kuwa atatumia misa hiyo kulaani vikali kitendo cha kinyama alichofanyiwa Tundu Lissu na watu hao wasiojulikana ambao waliweza kupiga gari lake zaidi ya risasi 30 huku risasi tano ndizo ziliweza kumjeruhi Mbunge huyo.

"Jumapili hii  Septemba 10, 2017 nitaongoza maombi maalumu ya kuombea Afya ya Mhe. Tundu Lissu na kulaani Vikali kitendo cha Kikatili na Kinyama alichofanyiwa. Maombi haya yatafanyika katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo Dar es Salaam tunawakaribisha wote watakaopenda kuungana nasi katika maombi haya" aliandika mchungaji Gwajima kupitia ukurasa wake wa facebook

Mchungaji Gwajima amekuwa akilaani mambo mbalimbali ambayo huwa yanatokea katika nchi kupitia misa mbalimbali ambazo huwa anafanyia katika kanisa lake hilo ikiwa pamoja na kuombea taifa amani na usalama. 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...