headlines

» » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?

SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 52
Tulipoishia, Nilianza kwa kularuriwa nguo kisha mmoja akaanza kwa kunicharanga miguuni. Niliangushwa chini kisha nikawa nang'atwa sehemu mbalimbali. Mara ikasikika sauti kama ya Peris ikisema______Songa nayo........ Heeey!! Simba achaa ghafla wale mbwa wakaniacha na kutoweka. Nikainuka kuangalia ni nani. Subhan Allah!!! Mbele yangu ilikuwa ni Peris mwenyewe. Nikamwangalia kwa macho ya mshangao na sura iliyojaa hasira kisha nikataka niinuke nikapambane naye. Hapo ndipo nilishindwa kusimama kwani nilikuwa nimeumizwa vibaya sana na wale mbwa.
Peris alianza kusogea karibu na nilikokuwa nimeketi. Alipokaribia kisha akaniambia, Yuu najua unaumia, najua unatamani kunifanya lolote baya, najua nilikuumiza kukuulia mwanao. Lakini jua kua si mimi nilimuua japo mpango wa kuuawa mwanangu nilikuwa naujua. Yuu nilikupenda sana ila mazingira na kazi yangu vilikuwa vunanibana kuwa karibu na wewe. Niliumia kila nilipoona unaonewa lakini ilinilazimu kufanya yote ili kukamilisha azma yangu. Nilikuwa mwanajeshi lakini hakuna hata mmoja kati yenu aliyekuwa akijua ukweli wa maisha yangu na hakuna aliyekuwa ananijuwa kwa undani.
Ukweli nilikuwa nao mimi na serikali yangu. Hakika nilikuonea sehemu nyingi sana. Pole kwa yote. Naongea haya yote kwasababu kazi yangu imefika mwisho na nimeikamilisha. Kilichobaki ni kuupeleka ushahidi mahakamani ili haki itendeke. Yuu bila mimi ungelikuwa umekufa zamani. Kuna sehemu zingine ulikuwa unastahili kuuawa lakini mimi nilisimama kidete kukutetea na kukupigania kwa mbinu za wizi. Ni kweli uliniona ni mbaya sana na nisiyekuwa na shukurani baada ya kugundua nafanya kazi na akina Zabroni Makweka. Lakini hili lilitokea mara baada ya kuteuliwa na wizara ya ulinzi kufanya upelelezi ndani ya kundi la majambazi.
Njia pekee ya kujua siri zao ilikuwa ni mimi kujiunga nao. Na kwakuwa niliapa kutotia siri za jeshi nililazimika kulinda kiapo changu hata kwa upanga. Pale ambapo nilitakiwa kuua ili nijiwekee mazingira ya kufanya kazi basi ilinilazimu sikuwa na jinsi. Niliumia wakati mwingine nilipoangamiza roho zisizo na hatia. Lakini lengo ilikuwa ni kuhakikisha kazi niliyotumwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania naimaliza kisha mambo mengine yafuate. Ilikuwa vigumu kukwambia kwani nilikatazwa na mkuu wangu wa kazi kumwambia yeyote. Hata leo nayasema haya kwasababu tuu nimefuatilia nyenendo zako tangu zamani ni kwamba sijaona lolote baya. Japo kuna kipindi ulianza kuacha njia kuu lakini ni kwasababu ya kudhulumiwa haki yako mara nyingi.
Kama binadamu mwenye moyo wa nyama na ninaeumia. Niliamua kukusaidia kwa kitu kimoja tuu. Kumwokoa baba yako najua itakuwa vigumu kuniamini tena ila ukweli ni kwamba mimi siyo jambazi wala siwezi kuwa jambazi. Naipenda Tanzania, nawapenda Watanzania kwaajili ya Tanzania nililazimika hata kuutumikisha mwili wangu lengo kupata habari za uhakika. Mda wote huo Peris akiongea mimi nilikuwa kimya tuu nikimsikiliza. Akaniambia Yuu baba yako niko nae na zaidi ushahidi wote kuhusu Zabroni na wewe kuwa huna hatia kwa lolote ninawo. Niliwarekodi katika matukio mbalimbali wakifanya mambo ya kinyama. Nilikuwa niitumia miwani iliyokuwa na kamera ndogo sana.
Nilifanikiwa kumteka Zabroni hata kufikia hatua ya kuniamini na kunipa uongozi ndani ya kundi la majambazi. Aliamini mimk ni polisi ninayesaliti jeshi na kulidharirsha vazi langu la uaskari. Kuna wakati alinitaka kimapenzi nililazimika kumpa ili tuu kazi yangu isiharibike. Kilichonisikitisha ni kuwa kuna mpaka viongozi wa kubwa kwenye sakata hili. Naomba nikuletee ushahidi hapa kama bado hautaniamini nitakuruhusu kunifanya lolote hata kunifinyangafinyanga ili uridhike nafsini mwako. Akainuka na kuingia ndani. Huku nyuma mimi nikawa nasikilizia maumivu ya kung'atwa na mbwa pia maneno makali aliyokuwa akiyaongea Perisi. Lakini nilijikaza kiume na vidonda vyangu huku nikiugulia na kujiaminisha kuwa Nitapona tuu.
Baada ya mda Perisi alirudi na bahasha kubwa kisha akamwaga vitu pale chini. Kulikuwa na vitu vingi sana pqle chini. Akaanza kunielezea kila kitu kilichokuwa kikioneka alianza kunionyesha cd mbalimbali akinambia zile ni sauti ambazo alifanikiwa kuwarekodi akina Zabroni wakipanga mipango mbalimbali juu ya kuua na kupora mali. Pia alikuwa na sura za bandia nyingi sana ambazi alidai kuwa ni za Zabroni na kundi lake. Ila kizuri ambacho yeye alinambia ni kuwa Zabroni hakuwahi kutumia sura ya bandia vile alivyo ndivyo alivyo hivo nisidhan sura yangu ilitumika bali ni ufanano mkubwa uliopo baina yangu na Zabroni.
Kulikuwa na vifaa vingi vya kiteknolojia. Ambavyo vilikuwa vya gharama sana. Peris aliendelea kusema. Ushahidi kwa sasa umekamilika na pale nitakapohakikisha nmewaweka ndani mtandao mzima nitqkuja kwako ili unifanye lolote. Hata kama utaniua nitapumzika kwa amani kwani roho yangu itajua kisasi kimelipwa. Mda huo wote pale ndani ya uwanja palitawaliwa na utulivu na ukimya huku mimi nikilia kwa maumivu. Peris alikuwa anaongea kwa uchungu sana mara ghafla_________
____________________________________________________________
____________________________________________________________
____________________Una lolote la kusema? Tukutane sehemu ya 53 coment yko muhmu chaaaaaoooooo.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
TANGAZO LA KAZI
»
Previous
SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...