headlines

    07:42 AM
» » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?


MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 53
Tulipoishia, Mda huo wote pale ndani ya uwanja palitawaliwa na utulivu na ukimya huku mimi nikilia kwa maumivu. Peris alikuwa anaongea kwa uchungu sana mara ghafla____Songa nayo.....Kuna mtu mwingine akaanza kutokea akiwa ametoka mle ndani. Nilimwangalia vizuri nikagundua ni baba yangu. Japo nilikuwa na maumivu lakini kwa furaha ya kumwona baba yangu nilifurahi nikajikuta nainuka na kumkimbilia baba yangu. Niliinuka kwa kuchechemea na kumfuata baba. Nikamkumbatia na kumbusu baba yangu. Machozi yalikuwa yakimtoka bila kikomo na mimi pia nililia sana nikimlilia baba yangu. Nilikuwa nalia machozi ya furaha.
Baada ya dakika kadhaa kupita baba aliniachia na kuwa kama asiyeamini. Baada ya kuniachia nilikaa chini kwani maumivu yalikuwa yananizidia. Ndipo baba akaanza kunieleza kilichomkuta mpaka kufikia pale alipo. Alianza kwa kusema mwanangu kwanza nashukuru kwa kutana na wewe, pili namshukuru huyu binti ambaye ndiye aliokoa uhai wangu. Ilikuwa niwe nimekufa. Cha tatu ni kuwa binti kanambia mambo mengi sana ikiwamo kuwa mumewahi kuishi pamoja kama mume na mke. Ameniambia kuwa mlijaliwa kupata mtoto kwa bahati mbaya alifariki. Poleni sana. Kikubwa si kutafuta mbaya kati yenu ni nani.
Tafuteni na unganisheni nguvu kumpigania adui aliye nje ya nyumba yenu. Kwasababu ya kiapo na kuipenda nchi binti alifanya mambo mengi. Amekuomba msamaha msamehe bure. Kwani ungali unakabiliwa na mtihani mzito mbele yako. Unapaswa kuikomboa nchi kutoka kwenye ujambazi.
Kwa kuwa nilikuwa naumia sana na nateseka kwa maumivu nikamkatisha baba kwa kusema naomba kwanza mniwahishe hospitali. Japo nikapate hata dawa ya kutuliza maumivu. Aliinuka haraka Peris na kukusanya vile vitu pale chini kisha akaniinua na kuniweka kwenye mikono yake. Peris alikuwa na nguvu sana. Alinibeba mpaka kwenye gari na kisha akanipakiza kisha baba naye akaingia na wakanikimbiza hospitali.
Nilifika hospitali na kupewa huduma kwa uzuri. Nipata huduma ya kunisaidia. Tulikuwa tumeoba chumba cha siri pale hospitalini kwani tulikuwa na mashaka ya kuwa mda wowote Zabroni na kundi lake wakijua tulipo usalama hakuna. Basi nilihudumiwa kwa siku mbili na ta tatu nilikuwa nimepona kwa kiasi kikubwa. Hapo ndipo madaktari walaniruhusu kutoka. Tuliambiwa tunaweza kuondoka mda wowote. Peris alinikabidhi ule ushahidi na kusema ile kazi tumefanya wote hivyo hata kuikabidhi wizara ya mambo ya ndani ikishirikiana na wizara ya ulinzi na usalama ni lazima tuwe wote.
Basi tulibaki mle hospitali huku tukikubaliana kuwa tutaondoka. Giza likiingia. Mule ndani ndipo baba kwa mbali alionekana kama aliyekuwa akisumbuliwa kitu kichwani. Nilimwangalia nikaona ni kweli hayuko sawa. Nikamwuliza baba vipi kuna tatizo? Ndipo baba akaiangalia kisha akainama na kusema ndio mwanangu kuna tatizo tena kubwa. Nilishtuka nikamwuliza kwa haraka tatizo gani.?
Peris akaniangalia kisha akamwangalia baba yangu. Kisha akauliza baba kuna nini? Baba alianza kama kulia hivi kisha akasema Yuu mwanangu najua mimi ni baba yako. Naumia sana kwa hili ninalokwenda kukwambia kwa sasa. Sijui utalichukuliaje ila huo ndio ukweli wa maisha ya ujana wangu. Sikuwa mwaminifu kwa mama yako. Nilikuwa na mahusiano na watu tofauti tofauti kona mbalimbali za nchi hii. Hali hii ilinifanya kuzaa hovyo. Zabroni Makweka si Zabroni Makweka Bali anaiwa Samweli. Ni kaka yako wa damu. Sikuwahi kukwambia hili pia kuna dada zako na kaka zako wengine zaidi ya watano. Najua nilikosea na nilimkosea mama yako. Zabroni wakati amefikisha umri wa miaka mitatu mama yake aliolewa na mtu mmoja tajiri sana ambaye inasemekana alikuwa nadangulo. Humo alikuwa anauza wanawake. Baada ya kuolewa naye ndio ikawa mwisho wa kumwona Samweli na nikaja kumwona kwenye magazeti.
Alikuwa akionekana ni mtoto wa huyo mtu aitwae Makweka. Nadhani huyu ndiye alibadili roho ya Samweli na kumpandikiza ujambazi mpaka kufikia hapo. Zabroni hamjui mama yake haijulikani mama yake yuko wapi kwani baada ya kumwoa inasemekana walitenganishwa. Hapo ndipo Samweli alipoteza mwelekeo wa maisha. Lakini yule ni kaka yako kabisaa. Najilaumuna najutia nafsi yangu kwa yote niliyoyafanya ujanani na kufanya madhara makubwa uzeeni. Tazama sasa ukweli unajulikana kipindi cha shida. Na......... Kabla hajaendelea tulikatishwa na dokta aliyeingia na kusema.
Samahani tumeambiwa mmeruhusiwa. Hivyo mnaweza kuondoka kwani chumba kinahitajika kutumika kwa sasa. Hivyo ni vyema tukampisha mgonjwa ambaye ni binadamu kama sisi. Tufanyeni ubinadamu basi. Japo najua nawasumbua na nawatesa lakini mtanisamehe kwa hilo. Mi nikajibu usijali mkuu. Basi nikamwomba Peris akaandae gari yake. Huku nyuma nikawa namnyamazisha baba kwani alikuwa akilia kwa uchungu sana. Machozi yalikuwa yakimtoka bila kikomo.
Baada ya mda Peris akarudi. Kisha akasema twendeni. Niliinuka na kuichukua ile bahasha yenye ushahidi wote. Kisha nikaitia kwenye begi. Huku kichwani wazo likianza kunijia je nimkamate kaka yangu? Tulitoka nikiwa natafakari hilo na tulipofika nje. Tuliikaribia gari mara ghafla wakatokea watu na kufyatua risasi ambazo zilimpata Peris kifuani na baba pia kisha_______________________________________________________
____________________________________________________________
_____________________________________Usikose sehemu ya 54 tujue yaliyojiriri huk

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?
»
Previous
Maneno aliyosema Tundu Lissu baada ya kuzinduka

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...