» » Selemani Jafo awataka Wakuu wa Wilaya kuitumia vizuri sheria ya kuweka ndani watu

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amewatakaa Wakuu wa Wilaya kuitumia vizuri sheria ya kumuweka mtu ndani kwa saa 48 pasipo uonevu wowote.

Jafo ameitoa kauli hiyo  Mjini Dodoma alipokuwa akifunga mafunzo ya Uongozi ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Ruvuma, Songwe, Shinyanga na Dar es Salaam, Yalioanza Septemba 11, mwaka huu.

"Fanyeni kazi kwa kufuata mipaka yenu ya kazi, kwani ndilo jambo pekee litakalo waepusha na migogoro katika maeneo yenu ya kazi," amesema Jafo.

Amesema , viongozi hao wanapaswa kufanya kazi pasipo kumuonea au kumpendelea mtu kwa namna yoyote ile, bali wakawe mifano kwa kujenga uhusiano mzuri na watumishi wanao waongoza pamoja na wananchi.

Jafo amewataka kwenda kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya rushwa na dawa za kulevya, usimamizi wa miradi ya maendeleo,matumizi ya mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali pamoja na kusimamia uwajibikaji wa watumishi wa umma.

Wakati wakiendelea na mafunzo hayo, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi amewatembelea Wakuu hao wa Wilaya na kuwapa miongozo ya utendaji kazi pamoja na mipaka ya kazi yao ili kuepuka migogoro katika maeneo yao ya kazi.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo kutoka Taasisi ya Uongozi, Kadari Singo alizitaja mada walizofundishwa viongozi hao kuwa ni pamoja na muundo wa Serikali, namna ya kumbadili kiongozi, utunzaji wa nyaraka na siri za Serikali, manunuzi, matumizi sahihi ya vyombo vya usalama, usalama wa nchi pamoja na mambo ya uchaguzi.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...