» » Mwijage Kutua India Kuisafisha Tanzania

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage  amekiri kupokea wito wa kwenda nchini India kwa ajili ya kusafisha jina la Tanzani baada ya watu wanaodaiwa ni madalali tapeli wa zao korosho kulichafua.

Mh. Mwijage ameyasema hayo jana ambapo amedai kuwa anaoushahidi  kuwa kampuni hizo za udalali zilichafua jina la nchi hivyo ni lazima awafikishe katika mikono ya sheria.

“Vitendo hivi vinavyofanywa na makampuni haya havivumiliki kwani mchezo huu ni mauti kwetu na nitahakikisha wanachukuliwa hatua kwani ninao ushahidi unaotosheleza,”alisema Mwijage.

Mh. Mwijage amefafanua kwa kusema kwamba watu wametapeliwa kwa kuambiwa pindi wanapoagiza mazao watoe pesa ya kianzio ambayo ni kuanzia dola za Marekani 123,000, sawa na Sh275 milioni na dola 200,000 sawa na Sh448milioni za kitanzania.

“Nimepokea wito kutoka India kwa ajili ya kwenda kusafisha jina la nchi kutokana na taswira iliyosababishwa na uwepo wa matapeli hao,”alisema Mwijage.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...