» » Diwani kurushiwa mishale wilayani Karagwe,Kagera.


Jeshi la polisi kwenye Wilaya ya Karagwe limewatia mbaroni watuhumiwa waliohusika kwenye shambulio la mikuki lililofanyika juzi dhidi ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Bw.Godfrey Mheruka na Diwani wa kata ya NyakahangaMhe.Charles Bechumila na inasemekana kuwa washambuliaji hao ni watoto na walinzi wa aliyetoa agizo la shambulio hilo.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya shambulio hilo linatokana na mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wananchi na mtu anayejulikana kwa jina la Kamiyandaambaye amejimilikisha ekari 152 za eneo hilo na pindi diwani alipoitisha mkutano wa kijiji bwana huyo alihisi ni mbinu za kumtoa yeye na hivyo kuwatuma watu hao kwa ajili ya shambulio hilo.

Diwani Bechumila aliyejeruhiwa kutokana na tukio hilo alichomwa mikuki minne maeneo ya shingoni, ubavuni, kifuani na kwenye paja na mpaka sasa bado anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Nyakahanga.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...