» » Huyu ndie Mwanamke anayetaka China kula wadudu

Huyu ndie Mwanamke anayetaka China kula wadudu

Haki miliki ya pichaRYAN LASH/TEDImage captionMwanamke wa China anayefanya kampeni za kula wadudu ili kuimarisha tabia za kula nchini humo.

Mfanyibiashara mmoja wa Uchina anafanya kampeni za kula wadudu ili kuimarisha tabia za kula nchini humo.

Matilda Ho alizungumza katika mkutano wa Teknonoljia, utumbuizaji na mitindo kuhusu umuhimu wa kusambaza ujumbe wa chakula chenye afya.

Anaunga mkono vyakula ikiwemo vile vilivyo na protini kutoka kwa viwavi.

China ina tatizo la ukuwaji kutokana na kunenepe kupitia kiasi na ugonjwa wa kisukari.

''China ina asilimia 20 ya watu duniani lakini ni aslimia 7 pekee ya ardhi yake ilio na rutba'', alisema bi Ho.

Mtu mmoja kati ya raia wanne wa Uchina anaugua ugonjwa wa kisukari na mmoja kati ya watu wanne amenenepa kupita kiasi.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionWadudu kwa jina Silkworms anaofanya kampeni kwa Wachina kuwala

Bi Ho alianza kukabiliana na swala hilo kupitia soko la mtandao la wakulima ambalo sasa linatoa bidhaa 240 kutoka kwa walkulima 57.

Mtandao huo umepata wateja 40,000 tangu uzinduliwe miezi 18 iliopita.

''Nilitaka kutumia teknolojia ili kupunguza pengo lililopo kati ya wakulima na wanunuzi'', bi Ho aliambia BBC.

''Ni haki yako kujua kule chakula chako kinakotoka na kuwahamasisha wateja''.

Chakula hicho husambazwa kwa wateja kupitia magari ya kielektroniki na maboksi.

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...