» » US: Mfumo wa kujilinda ''utamuamsha'' rais wa K. Kaskazini

US: Mfumo wa kujilinda ''utamuamsha'' rais wa K. Kaskazini

Haki miliki ya pichaAFPImage captionUpelekaji wa mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini ulipingwa na waandamanaji

Mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Marekani unaowekwa nchini Korea Kusini utaanza kufanya kazi katika siku chache zijazo, jeshi la Marekani limesema.

Mfumo huo wa Thaad umetengezwa kuilinda Korea Kusini na majeshi ya Marekani yaliopiga kambi nchini humo dhidi ya vitisho vya Korea Kaskazini.

Vifaa vya mfumo huo vilipelekwa katika taifa hilo siku ya Jumatano, Admirali Harry Harris ambaye ni ni kamanda wa eneo la Pacific alisema kuwa Thaada itaanza kufanya kazi katika siku chache zijazo ili kuiinda Korea Kusini dhidi ya vitisho vya jirani yake Korea kaskazini.

Korea Kaskazini yaonywa na MarekaniTrump aionya tena Korea KaskaziniKorea Kaskazini yarusha makombora tena

Amesema kuwa mfumo huo unalenga ''kumfungua macho'' rais Kim Jong un na ''sio kumuangusha''.

Image captionMakombora yanayomilikiwa na Korea Kaskazini

Wizara ya ulinzi baadaye ilithibitisha kwamba mfumo huo utaanza kufanya kazi hivi karibuni.

Msemaji amesema kuwa uwepo wa vifaa unamaanisha kwamba Korea Kusini na Marekani zina uwezo kukabiliana na uchochezi wa Korea Kaskazini.

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...