» » Wakenya milioni 19 kupiga kura Leo Kuchagua Rais na Viongozi Wengine

Wakenya milioni 19 wanashiriki kwenye uchaguzi wa kihistoria leo

Kiongozi wa chama tawala cha Jubilee, Rais Uhuru Kenyatta, anachuana tena na hasimu wake wa kisiasa, Raila Odinga wa muungano mkuu wa upinzani, NASA, kwenye kinyang'anyiro kinachotazamiwa kuwa cha vuta ni kuvute baina ya wawili hao, licha ya kuwepo wagombea wengine saba wa urais.

Uchaguzi huo unaowagharimu walipakodi wa Kenya shilingi bilioni 49 unaelezwa kuwa ghali zaidi ikilinganishwa na uchaguzi katika mataifa jirani.

Zaidi ya wagombea 1,000 watachaguliwa na Wakenya kwenye nafasi za urais, ugavana, useneta, ubunge, uwakilishi wa akinamama na wa kaunti mbalimbali.

Kuna vituo elfu 40,883 vya kupigia kura vitakavyolindwa na maafisa 150,000 wa idara za usalama, na zaidi ya waangalizi 9,000 wa kitaifa na wa kigeni wameidhinishwa kuangalia uchaguzi huu.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...