![]() |
Barabara hiyo imeanza kuchimbika na lami kubanduka na kubaki vumbi licha ya kufanyiwa ukarabati wakati wote wa kila mwaka.
Ubovu wake ni kujaa mashimo yanayochangia magari yenye mizigo kushindwa kuendelea na safari, huku mengine yakipinduka baada ya kupanda milima na hata kurudi nyuma.
|


![]() |
Wakizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu katika eneo hilo, baadhi ya madereva wamesema eneo hilo ni bovu miaka yote na unapofanyika ukarabati, wakandarasi wanatumia saruji rojorojo bila kuzingatia kuwa magari yanayopita yanakuwa na tani nyingi za mizigo.
Wamesema magari hayo yanasafiri kutoka na kuingia Dar Es Salaam hadi Rwanda na Burundi na hata Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, kwa kuingiza fedha zinazoweza kuinua uchumi wa Taifa, hivyo serikali ya Tanzania haina budi kujenga upya barabara hiyo, kutoka Nyakanazi wilayani Biharamulo hadi Rusumo Wilayani ya Ngara mkoani Kagera.
|


![]() |
Kukwama kila wakati kwa magari katika eneo hilo la Nyabugombe , safari za magari ya abiria kutoka Ngara kwenda mikoani kupitia eneo la barabara hiyo zimekuwa zikisimama kwa saa kadhaa huku huduma za kijamii kama maji, mighahawa ya kuuzia chakula , zahanati na mawasiliano ya mitandao ya simu za mkononi vikikosekana na kuleta changamoto kwa wasafiri.
Hata hivyo Mhandisi wa barabara wa mkoa wa Kagera Bw.Chakindo Nasiri, alipotafutwa kwa njia ya simu amesema barabara hiyo inahitaji kujengwa upya, na kinachofanyika hivi sasa ni ukarabati mdogo ili kuwezesha magari kupita kusafirisha bidhaa kuelekea nchi za Rwanda. Burundi na DRC.
Picha Na Shaban Ndyamukama.
|
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment