» » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?SEHEMU YA 50


MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 50
Tulipoishia, Naingia humo kama nikifa kwaheri na kama nitapona basi Peris kwaheri. Nikaachomoa kisu changu na kisha nikaingia kwa kasi mara ghafla________Songa nayo...... Nikashanga nashikwa bega kwa namna ya mtu kunizuia hapo ndipo ilikuwa kosa kubwa kwani waliamsha hadira zilizowaka kama moto wa kifuu. Niligeuka bila kuangalia ni nani aliyenishika niligeuka na kisu na kujikuta nimemchoma maeneo ya shingo. Peris alipogeuka akashtuka na kuanza kutafuta sehemu ya kukimbilia. Nikawahi mlangoni na kuuzuia asije akatoka kuona vile Peris akatoa kidonge fulani akanywa na kuanguka.
Nikajua tuu ni ile tabia ya majbazi kujiua ili kukwepa kuhojiwa kwahiyo hata Peris atakuwa kameza kkdonge cha sumu. Nilijilaumu kwa kukosa hata kumpiga Peris kwani lengo langu ilikuwa nimpige hata kiasi ili nipunguze uchungu. Lakini kwakuwa aliamua kujiua nikaona siyo mbaya kwakuwa kazi yangu inazidi kupungua na mwisho wa siku wote wataisha tuu.
Nikarudisha kisu changu kwenye miguu nilikokitoa kisha nikaanza kuwaza zile maiti nazifanyaje. Nikageukia upande wa pili huku nikiwaza kwa kwenda kuzitupa. Nikiwa nimejiachia na kulegea nikijua wote wamekufa ghafla nikisukumwa kwa nguvu za ajabu kabsa nikaangukia kwenye meza.Bila kujizua. Ghafla nilipogeuka nikamwona ni Peris anatoka mbio. Haa! Kumbe alinichezea mchezo hakumeza sumu!
Nikajichanganya kwa nyuma na kuanza kumfukuzia. Kama kawaida Peris alikuwa anajua kukimbia jamani alikimbia akaniacha nyuma naye akapotea kwenye vichochoro vya moja ya mitaa ya jiji la Dar es salaam. Nilimtafuta kwenye vichochoro vile vya ule mtaa bila mafanikio yoyote. Nilijiona mjinga sana niliyekurupuka kuamini kama Peris kafa kumbe hakufa. Wakati natafakari nifanye nini niliamua kurudi nyumbani na kujipanga upya.
Nikatembea hadi nyumbani ambapo nilifika na nijashangaa maiti ile siioni. Hapo nikagundua tayari mle si mahali salama wamesha nichora. Nikaingia ndani na kujikusanyia baadhi ya vitu vyangu vya muhimu na kuamua kuondoka eneo lile. Lakini wakati nakusanya kuna mkoba wa Peris aliusahau wakati anaondoka nikauchukua na kuanza kuupekua.
Nikikutana na vitu vingi sana vilivyokuwa pasua kichwa kwa maswali. Kwani kuna mikataba niliona amesaini yeye pamoja na naibu waziri wa ulinzi Tanzania. Ambayo ilionyesha kuna kazi ametumwa na taifa na anatakiwa kuifanya kwa siri kubwa. Pia niliona kitambulisho kilichomtambulisha kama mpelelezi wa siri. Mmmh! Ilikuwa mshituko kidogo kwani nilibaki nashangaa inamana Peris ni mpelelezi wa siri? Je anampeleleza nani? Mbona kama ni akina Zabroni anashirikiana nao?
Yalikuwa maswali mengi yaliyokosa majibu. Nikaamua kuondoka zangu eneo hilo na kutafuta maficho mapya. Nilienda sehemu mpya huku nikiwaza baba yangu yuko wapi? Nilijificha eneo fulani huku nikiwa na ule mkoba wa Peris. Kuna wazo likanijia niendelee kuupekua ndipo nikaanza tena kuupekua. Nilikutana na vitu vingi sana vya kijeshi.
Nilikuwa najiuliza maswali juu ya Peris kwani niakawa naumiza kichwa kujiuliza inamana Jeshi la polisi linatambua uwepo wa Peris. Mmmh potelea mbali kikubwa mimi nimalize kazi yangu basi nitamuua Peris, nitamuua Zabroni, kisha nitawauwa wote wanaohusika na ujambazi kisha nitajisalimisha mikononi mwa polisi ili kama nikuhukumiwa nihukumiwe kwa amani.
Nililala pale kisha asubuhi nikaamka na kuanza mishemishe zangu za kutafuta majambazi. Niliingia mitaani nikimtafuta Zabroni kwani kuna sehemu ilikuewa ni lazima apatikane nilianza safari kuelekea huko na nilipofika nilikaa sehemu fulani ili kumlia mingo. Nilikaa kwa mda fulani na kumsubiri ili kama akipita eneo lile nimalize kazi yangu kabsaaa.
Nilikaa mda mrefu bila mafanikio na mpaka nikaanza kukata tamaa n a kuamua kuondoka zangu kurudi nyumbani. Nikainuka na kuanza safari kuelekea nyumbani ambako ndipo yalipo maficho yangu mapya. Nilitoka pale na huku kichwa kikiuma na kuwaza na kuwazua jinsi gani nitamaliza ile kazi maana ilianza kuonekana ngumu wakati naelekea mwishoni kuwamaliza.
Nikiwa njiani nikageuka kwa nyuma na kumkuta kama mtu ninayemfahamu hivi. Nikaamua kugeuka vizuri ndipo nilipomwona Zabroni akikatza eneo lile akielekea mahali fulani. Hapo ndipo nikaamua moja tuu ni kumfukuza mpaka nimpate. Nilijiweka sawa nikaanza kumfuatilia kwa nyuma.
Inavyoonekana hata yeye aliniona kwani alikuwa akitembea kwa mawenge sana. Nikazidi kumkazia mwendo naye akazidisha mpaka tukajikuta tumetoweka katikakati ya kundi la watu sasa ni sisi wawili tumebaki. Nikaanza kumkimbiza. Chaajabu naye alianza kukimbia kuelekea bonde fulani hivi. Sikukata tama nikazidi kuongeza juhudi na kujituma na kujiapiza nikimkuta halali yangu.
Zabroni alikimbia na kufika sehemu kisha akasimama. Nilishtuka na kujiuliza kwanini amesimama ghafla. Hali ile ilinitisha kidogo lakini nikajipa moyo. Nikachomoa kisu na kuanza kumfuata. Chaajabu alikuwa hata hageuki kuniangalia. Nikajua hapa kuna namna lakini nikasema mpaka nimuue hata kama nitakamatwa. Nilimfuata mpaka nilipomkaribia na kuinua kisu kumchoma ghafla________________________
____________________________________________________________
____________________________________________________________
_________________________________________Tukutane sehemu ya 51 tujue mapyaaa yaliyojiri. Usisahau kulike Fan page yetu Simulizi za Mwalimu Yusuph tupate kujuana zaidi Chaoooooo.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...