» » Rais Magufuli, Dangote, Obama kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Kenyatta


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Magufuli na Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria katika sherehe za uapisho wa Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Kamati ya maandalizi ya sherehe hizo inayoongozwa na Katibu Kiongozi, Joseph Kinyua imebainisha kuwa imeandaa orodha ya majina ya viongozi wa kimataifa kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la kihistoria la uapisho wa Kenyatta endapo ushindi wa Kenyatta hautopingwa mahakamani.

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, sherehe za uapisho hufanyika siku 14, baada ya mshindi wa uchaguzi kutangazwa ili kutoa fursa kwa chama chochote kinachotaka kupinga matokeo kufanya hivyo.

Viongozi wengine wanaotarajiwa kualikwa katika sherehe hizo wakiwemo wakuu wa nchi ni pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Wengine ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May.

Aidha, katika orodha hiyo pia yupo Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, mfanyabiashara tajiri namba moja Afrika Aliko Dangote, Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia, Aga Khan, Waziri Mkuu mstaafu wa Italia, Matteo Renzi na Rais Xi Jinping wa China.

“Tupo kwenye maandalizi ya sherehe za uapisho wa Rais wakati tukisubiria hatua za kikatiba kukamilika. Orodha hii ni ya marafiki wa Kenyatta, viongozi wa Afrika na viongozi wengine wa kimataifa, tunaotarajia kuwaalika”, amesema mmoja wa wanakamati hiyo ya maandalizi.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi Kenya, Wafula Chebukati mwishoni mwa wiki alimtangaza rasmi Rais Kenyatta na Naibu wake, William Ruto kuwa washindi katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita nchini humo.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...