» » Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) laonywa jinsi lilivyomaliza mgogoro wa Makonda na Clouds.

Kufuatia maoni ya baadhii ya watu mbalimbali na waandishi wa habari kutoridhika na maamuzi ya Jukwaa la Wahariri (TEF), viongozi wamepewa onyo la kutorudia makosa baada ya kukiri.

Katika mkutano mkuu uliofanyika Agosti 13, viongozi hao walikiri kuitisha mkutano na waandishi wa habari Agosti 9 bila ya kupata idhini.

Hatua hiyo ilisababisha kujengeka kwa taswira mbaya kiuwajibikaji, kanuni na utaratibu.

Katika taarifa ya Mwenyekiti Maalum wa TEF, Walace Mauggo imeeleza kuwa jukwaa kwa kauli moja limetoa onyo kwa viongozi wake kutorudia yale ambayo yamejitokeza.

“Baada ya kutafakari na kutathmini mwenendo wa mkutano huo, jukwaa lilobaini kuwepo kwa kasoro kubwa wakati wa kurejesha mahusiano wa kikazi na kiongozi ambaye habari zake zilizuiwa kuripotiwa kwa takribani miezi mitano,”imeeleza taarifa hiyo.

Pia wametakiwa kuhakikisha kunapotokea masuala makubwa kama hayo ambayo yashafanyiwa maamuzi na mkutano mkuu na taasisi nyingine za habari yanarudiswa maamuzi kwa wanachama kabla ya hatua za  mwisho.

Mauggo ameeleza kuwa TEF haitasita kuchukua hatua kwa kiongozi au mtu yoyote atakayeonekana kutishia usalama wa wanahabari, uhuru wa uhariri na vyombo vya habari.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...