» » Nikiteuliwa na Rais Magufuli nitakataa

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa hatokubali endapo Rais Dkt Magufuli atamteua kushika nafasi yoyote ya uongozi kwani hatakuwa na fursa ya kukijenga chama chake ili kiwe tayari kushinda uchaguzi na kushika dola.

Zitto ambaye chama anachotoka tayari kimetoa viongozi wawili ambao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Elisha Mghwira alisema endapo atateuliwa, atamshukuru Rais na kukataa uteuzi huo.

Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Mwananchi wakati akijibu swali kuhusu uteuzi wa viongozi wa chama chao ambao mmoja alikuwa mshauri wa chama na mwingine alikuwa mwenyekiti wa chama hicho kichanga Tanzania.

“Sitakubali uteuzi kwa sababu jukumu langu na viongozi wengine wa ACT- Wazalendo ni kujenga chama ili kupata ushawishi  na kuungwa mkono na umma na hatimaye kushika dola,” alisema Zitto.

“Kukubali uteuzi utakaoniondoa na kuniweka kando kwenye jukumu na malengo hayo ni kufifisha matumaini ya maelfu ya wana-ACT Wazalendo,” aliongeza Zitto.

Akizungumzia sababu za chama kuridhia uteuzi wa Prof. Mkumbo, Zitto alisema kwamba hapo hali ilikuwa ni tofauti kwa sababu kabla na baada ya uteuzi wa Mkumbo, yeye ni mtumishi wa umma, hivyo uteuzi wake haukushtua.

“Mama Anna Mghwira alikuwa ni mwanasiasa kwa nafasi yake ya uenyekiti Taifa, ndio maana tulimuondoa ili kumpa fursa kutumikia serikali.”

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...