» » Korea Kaskazini Yarusha Kombora Zito Katika Anga la Japani........Ni Siku Chatu Baada ya Japani Kudai Inauwezo wa Kuyatungua Hayo Makombora

Korea kaskazini imerusha makombora yake ambayo yalipita Japan kabla ya kudondokea baharini.

Makombora hayo yalisafiri kuelekea mashariki karibu kilomita elfu moja juu ya kisiwa cha Japan cha Hokkaido.

Tukio hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake.

Hakuna juhudi zilizofanywa na Japan kulitengua kombora hilo licha ya hapo awali kudai kuwa ilikuwa na uwezo huo, na badala yake  ilitoa onyo la kiusalama ikiwaambia raia wake katika eneo la Hokkaidokujificha chini ya majumba yaliojengwa ardhini.

Wanajeshi wa Marekani na Japan wanafanya zoezi la pamoja katika eneo hilo la Hokkado.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ameagiza uwezo wa utumiaji  nguvu ili kujibu shambulio hilo.Ndege nne za Korea Kusini zilifanya zoezi la kurusha makombora jana.

Bwana Abe alisema kuwa amezungumza na rais wa Marekani Donald Trump na kwamba wote wamekubaliana kuiongezea vikwazo  Korea Kaskazini.

Katika mfululizo wa majaribio yake ya makombora ya hivi karibuni Korea kaskazini haijawahi kurusha makombora yaliyopita juu ya ardhi ya nchi hiyo, hivyo tukio hili la sasa limeleta wasiwasi mkubwa.

Katika siku za hivi karibuni, Korea Kaskazini  ilijaribu kombora lake lililopata mafanikio kutokana na uwezo wake wa kuweza kuifikia Marekani na kuonyoa kuwa inasimamia mipango yake ya kushambulia kwa makombora eneo la Marekani la Guam, kilomita elfu mbili kusini mashariki mwa Japan.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...