» » Christopher Wray athibitishwa kuwa mkuu mpya wa FBI

Christopher Wray athibitishwa kuwa mkuu mpya wa shirika la ujasusi la FBI

Image captionChristopher Wray athibitishwa kuwa mkuu mpya wa shirika la ujasusi la FBI
Bunge la Seneti nchini Marekani limepiga kura ya kuthibitishwa Bwana Christopher Wray kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani la FBI.
Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu James Comey alipotimuliwa na Rais Donald Trump mwezi May kufuatia uchunguzi aliokuwa akiufanya kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo uliompa ushindi Rais Trump.
Christopher Wray ni mmoja wa maafisa wa ngazi za juu wa mahakama ya nchi hiyo ambaye alifanya kazi chini ya Rais George Bush.
Bwana Wray amepata uungwaji mkono kutoka vyama vyote kwenye Kamati ya Sheria ya Bunge la Seneti wakati wa kikao cha kuthibitishwa kilichoketi mwezi uliopita ambapo alionyesha kuitii Katiba.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...