» » Trump: Wanaobadili jinsia hawawezi kuhudumu katika jeshi


Haki miliki ya pichaEPAImage captionWakereketwa wa jinsia moja pamoja na wale wanaobadili jinsia zao hutumia bendera hizi

Rais Trump ametangaza kuwa Jeshi la Marekani halitawaruhusu watu wanaobadilisha jinsia zao kuendelea kufanya kazi ya aina yoyote jeshini.

Katika taarifa kadhaa kwenye mtandao wa Twitter, Bwana Trump alisema kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kufanya mashauriano na maafisa wa vyeo vya juu jeshini.

Alisema watu wanaobadilisha jinsia zao wataligharimu jeshi kimatibabu na kuvuruga maisha ya kawaida jeshini.

Mapema mwezi huu waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis, alisimamisha uajiri wa watu wanaobadilisha jinsia zao kwa miezi sita.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles